Skip to content

Yesu Anaosha Miguu ya Wanafunzi Wake

13 Ilikuwa siku moja kabla ya sikukuu ya Pasaka. Yesu alijua ya kuwa wakati wake wa kuondoka duniani na kurudi kwa Baba yake umekaribia. Alikuwa amewapenda sana wafuasi wake hapa duniani, akawapenda hadi mwisho.

Na wakati alipokuwa akila chakula cha jioni pamoja na wanafunzi wake, shetani alikuwa amekwisha kumpa Yuda Iskariote, mwana wa Simoni, wazo la kumsaliti Yesu. Yesu akijua ya kwamba Baba yake alikwisha mpa mamlaka juu ya vitu vyote; na kwamba yeye alitoka kwa Mungu na alikuwa anarudi kwa Mungu, alitoka mezani akaweka vazi lake kando, akajifunga taulo kiunoni. Kisha akamimina maji katika chombo akaanza kuwaosha wanafunzi wake miguu na kuikausha kwa ile taulo aliyojifunga kiu noni.

Alipomfikia Simoni Petro, Petro akamwambia, “Bwana, wewe unaniosha miguu?”

Yesu akamjibu, “Hivi sasa huelewi ninalofa nya lakini baadaye utaelewa.”

Petro akamjibu, “La, hutaosha miguu yangu kamwe!”

Yesu akamwambia, “Kama sitaosha miguu yako, huwezi kuwa mfuasi wangu.”

Ndipo Petro akasema, “Kama ni hivyo Bwana, nioshe miguu yangu pamoja na mikono yangu na kichwa changu pia!” 

10 Yesu akamwambia, “Mtu aliyekwishaoga ni safi mwili mzima naye hahitaji tena kunawa ila kuosha miguu tu. Ninyi nyote ni safi, isipokuwa mmoja.” 11 Yesu alifahamu ni nani angemsaliti, ndio sababu akasema, “Ninyi nyote ni safi, isipo kuwa mmoja.”

12 Alipomaliza kuwaosha miguu alivaa tena vazi lake, akarudi alipokuwa amekaa, ndipo akawaambia, “Je, mnaelewa maana ya jambo nililowafanyia? 13 Ninyi mnaniita mimi, Mwalimu na Bwana, na hii ni sawa, kwani ni kweli. 14 Kwa hiyo ikiwa mimi niliye Bwana wenu na Mwalimu wenu nimewaosha miguu, ninyi pia hamna budi kuoshana miguu. 15 Mimi nimewaonyesha mfano, ili mtendeane kama nilivyowafanyia. 16 Ninawaambia hakika, mtumishi hawezi kuwa mkuu kuliko bwana wake; wala anayetumwa hawezi kuwa mkuu kuliko aliyemtuma. 17 Kwa kuwa sasa mnafahamu mambo haya, mtabarikiwa na Mungu ikiwa mtayafanya.

Yesu Anatabiri Usaliti Wake

18 Siwazungumzii ninyi nyote. Ninawa fahamu wote niliowachagua. Maandiko yaliyotamka, ‘Yeye aliyekula chakula pamoja nami amekuwa msaliti wangu,’ hayana budi kutimia.

19 Ninawaambia mambo haya kabla hayajatokea ili yatakapotokea mpate kuamini ya kuwa mimi ndiye Kristo. 20 Nawahakikishia kuwa mtu anayemkubali na kumpokea ye yote ninayemtuma, ananipokea mimi. Na mtu anayenikubali na kunipokea, anampokea Baba yangu ambaye amenituma.”

21 Baada ya haya Yesu alifadhaika sana moyoni, akasema, “Ninawaambia wazi, mmoja wenu atanisaliti.”

22 Wanafunzi wake wakatazamana kwa wasiwasi, kwa kuwa hawakujua anamsema nani. 23 Mmoja wa wanafunzi ambaye Yesu alimpenda sana alikuwa amekaa karibu sana na Yesu. 24 Kwa hiyo Simoni Petro akamwashiria yule mwanafunzi akamwambia, “Tuambie, ni nani anayemsema.”

25 Yule mwanafunzi akimwegemea Yesu akamwambia, “Tafadhali Bwana tuambie, ni nani unayemzungumzia?”

26 Yesu akajibu, “Ni yule nitakayempa hiki kipande cha mkate baada ya kukichovya.” Kwa hiyo baada ya kuchovya ule mkate akampa Yuda, mwana wa Simoni Iskariote. 27 Mara tu baada ya kukipokea kile kipande cha mkate, shetani akamwingia moyoni.

Yesu akamwambia Yuda, “Jambo unalok wenda kufanya, kalifanye haraka.’ 28 Hakuna hata mmoja wa wale wengine waliokuwepo pale mezani aliyeelewa maana ya maneno aliy otamka Yesu. 29 Baadhi yao walidhani kwamba alikuwa anamwagiza akanunue vitu watakavyohitaji kwa ajili ya sikukuu au awape mas kini cho chote, kwa kuwa yeye alikuwa mtunza fedha. 30 Kwa hiyo mara baada ya kupokea ule mkate, Yuda alienda zake nje. Wakati huo giza lilikwisha ingia.

Yesu Anatabiri Kukana kwa Petro

31 Yuda alipokwisha ondoka, Yesu akawaambia, “Wakati ume karibia ambapo watu wataona utukufu wangu mimi Mwana wa Adamu na kwa njia hii watu watauona utukufu wa Mungu. 32 Na ikiwa Mungu atatukuzwa, yeye atanipa mimi utukufu wake, na atafanya hivyo mara.

33 Wapendwa wangu, muda wangu wa kuwa pamoja nanyi umekar ibia kwisha. Mtanitafuta; na kama nilivyowaambia Wayahudi, nina waambia na ninyi: ‘ninapokwenda hamwezi kunifuata’.

34 Nina waachia amri mpya: pendaneni ninyi kwa ninyi. Kama mimi nilivy owapenda, na ninyi mpendane vivyo hivyo. 35 Kama mkipendana hivyo, watu wote watafahamu ya kuwa ninyi ni wanafunzi wangu.”

36 Simoni Petro akamwuliza, “Bwana, kwani unakwenda wapi?”

Yesu akamjibu, “Ninapokwenda hamwezi kunifuata sasa, lakini mtanifuata baadaye.”

37 Petro akamwuliza tena, “Bwana, kwa nini siwezi kukufuata sasa? Mimi niko tayari kufa kwa ajili yako.”

38 Yesu akamjibu, “Je, ni kweli uko tayari kutoa maisha yako kwa ajili yangu? Ninakwambia hakika ya kuwa, kabla jogoo hajawika, utakanusha mara tatu kwamba hunijui.”

Yesu Awafariji Wanafunzi Wake

14 Yesu akawaambia, “Msifadhaike mioyoni mwenu. Mwaminini Mungu, niaminini na mimi pia. Katika nyumba ya baba yangu mna nafasi nyingi. Kama sivyo, nisingeliwaambia kwamba nakwenda kuwaandalia makao. Na nikishawaandalia, nitarudi kuwachukua mkae pamoja nami; ili mahali nilipo, nanyi mpate kuwepo. Ninyi mnajua njia ya kufikia ninakokwenda.”

Yesu Njia ya kwenda kwa Baba

Tomaso akamwuliza, “Bwana, hatujui unakokwenda; tutaijuaje njia?”

Yesu akawaam bia, “Mimi ndiye Njia na Kweli na Uzima; mtu hawezi kufika kwa Baba bila kupitia kwangu. Kama mngekuwa mnajua mimi ni nani, mngemfahamu na Baba yangu. Tangu sasa mnamfahamu Baba yangu na mmemwona.”

Filipo akamwambia Yesu, “Bwana, tuonyeshe Baba yako nasi tutaridhika.”

Yesu akamjibu, “Filipo, imekuwaje hunifahamu baada ya mimi kuwa pamoja nanyi muda wote huu? Mtu ye yote ambaye ameniona mimi, amemwona Baba. Sasa inakuwaje unasema, ‘Tuonyeshe Baba’? 10 Je, huamini ya kuwa mimi niko ndani ya Baba yangu, na Baba yangu yuko ndani yangu? Mambo ninayowaambia siyasemi kwa mamlaka yangu mwenyewe, bali yanatoka kwa Baba yangu ambaye anaishi ndani yangu, na ndiye anayetenda haya yote. 11 Niaminini ninapowaambia ya kuwa mimi ni ndani ya Baba yangu na Baba yangu yu ndani yangu. La sivyo, niaminini kwa sababu ya haya mambo ninayotenda. 12 Ninawaambia hakika, mtu ye yote akiniamini ataweza kufanya miujiza kama hii na hata zaidi, kwa kuwa mimi ninakwenda kwa Baba yangu. 13 Kitu cho chote mtakachoomba kwa jina langu, nitawafanyia, ili Baba yangu apate kutukuzwa kwa yale ambayo mimi Mwanae nitawafanyia. 14 Mkiniomba cho chote kwa jina langu nitawafanyia.”

Yesu Anaahidi Roho Mtakatifu

15 “Kama mnanipenda mtatimiza amri zangu. 16 Nami nitam womba Baba, naye atawapeni Msaidizi mwingine akae nanyi siku zote. 17 Huyo ndiye Roho wa Kweli ambaye watu wasioamini hawawezi kumpokea. Watu kama hao hawamwoni wala hawamfahamu. Ninyi mnamfahamu kwa kuwa anakaa ndani yenu na ataendelea kuwa nanyi. 18 Sitawaacha kama yatima. Nitarudi kwenu. 19 Baada ya muda mfupi watu wa ulimwengu hawataniona tena, ila ninyi mta niona; na kwa kuwa mimi ni hai, ninyi pia mtakuwa hai. 20 Wakati huo utakapofika mtajua ya kuwa mimi niko ndani ya Baba yangu na ninyi mko ndani yangu. 21 Mtu anayezishika amri zangu na kuziti miza ndiye anayenipenda. Na mtu anayenipenda, Baba yangu atam penda; nami nitampenda na kujidhihirisha kwake.”

22 Yuda, siyo Iskariote, akamwuliza, “Bwana, itakuwaje ujidhihirishe kwetu tu na si kwa ulimwengu mzima?”

23 Yesu akamjibu, “Mtu akinipenda atashika mafundisho yangu na Baba yangu atampenda, nasi tutafanya makao yetu kwake. 24 Mtu asiyenipenda hayashiki mafundisho yangu na mafundisho niliyowapeni si yangu bali yametoka kwa Baba yangu aliyenituma.

25 “Nimewaambia mambo haya wakati nikiwa bado nipo nanyi. 26 Lakini yule Msaidizi, yaani Roho Mtakatifu, ambaye Baba yangu atamtuma kwenu kwa jina langu, atawafundisha mambo yote, na kuwakumbusha yote niliyowaambia. 27 Ninawaachia amani. Nawapeni amani yangu; amani hii ulimwengu hauwezi kuwapa. Msifadhaike mioyoni mwenu, wala msiogope.

28 Kumbukeni nilivyowaambia, ‘Ninakwenda, na nitarudi.’ Kama kweli mngalinipenda mngefurahi, kwa kuwa nakwenda kwa Baba; na Baba yangu ni mkuu kuliko mimi. 29 Na sasa nimewaambia mambo haya kabla hayajatokea ili yataka potokea mpate kuamini. 30 Sitasema tena mengi nanyi kwa sababu mtawala wa dunia hii anakuja. Yeye hana uwezo juu yangu. 31 Lakini ninatii amri ya Baba ili ulimwengu upate kujua kwamba nampenda Baba.

Simameni tuondoke hapa.’

Mzabibu na Matawi

15 ‘Mimi ni mzabibu wa kweli na Baba yangu ndiye mkulima. Kila tawi ndani yangu lisilozaa matunda, Baba yangu hulikata; na kila tawi lizaalo, yeye hulisafisha ili lipate kuzaa matunda zaidi. Ninyi mmekwisha kuwa safi kwa sababu ya mafundisho nili yowapa. Kaeni ndani yangu nami nikae ndani yenu. Kama vile tawi lisivyoweza kuzaa matunda pasipo kuwa sehemu ya mzabibu, vivyo hivyo, ninyi msipokaa ndani yangu hamwezi kufanya lo lote.

Mimi ni mzabibu; ninyi ni matawi; anayekaa ndani yangu nami ndani yake, huyo huzaa matunda mengi sana; maana pasipo mimi ninyi hamwezi kufanya lo lote. Mtu asipokaa ndani yangu hutupwa nje kama tawi na kunyauka. Matawi hayo hukusanywa na kutupwa motoni, yakateketea. Ninyi mkikaa ndani yangu na maneno yangu yakikaa ndani yenu, ombeni lo lote mtakalo nanyi mtatendewa. Mnapozaa matunda kwa wingi Baba yangu anatukuzwa, na hivyo mnadhihirisha kuwa ninyi ni wanafunzi wangu.

“Kama Baba alivyonipenda mimi, hivyo ndivyo mimi nilivy owapenda ninyi; dumuni katika pendo langu. 10 Mkizishika amri zangu mtakaa ndani ya pendo langu kama mimi nilivyozishika amri za Baba yangu na kukaa katika pendo lake. 11 “Nimewaambia haya kusudi furaha yangu iwe ndani yenu, nanyi mpate kuwa na furaha iliyokamilika. 12 “Amri yangu ni hii: pendaneni kama nilivyowapenda. 13 Hakuna mtu mwenye upendo unaozidi ule wa mtu anayejitoa afe kwa ajili ya rafiki zake. 14 Ninyi ni rafiki zangu ikiwa mtafa nya ninayowaagiza. 15 Siwaiti ninyi watumishi tena kwa sababu mtumishi haelewi shughuli za bwana wake; bali nimewaita rafiki, kwa maana mambo yote niliyoyasikia kutoka kwa Baba yangu nimewa fahamisha. 16 Hamkunichagua, bali mimi nimewachagua ninyi na nimewatuma mwende mkazae matunda, na matunda yenu yapate kudumu, ili lo lote mtakalomwomba Baba katika jina langu, awatimizie. 17 Hii ndio amri yangu: pendaneni.

Ulimwengu Unawachukia Wanafunzi

18 “Kama ulimwengu ukiwachukia, fahamuni kwamba ulinichukia mimi kabla haujawachukia ninyi. 19 Kama mngekuwa watu wa ulim wengu huu, ulimwengu ungeliwapenda. Ulimwengu unawachukia kwa sababu ninyi si wa ulimwengu huu na mimi nimewachagua kutoka katika ulimwengu. 20 “Kumbukeni lile neno nililowaambia, ‘Hakuna mtumishi aliye mkuu kuliko bwana wake.’ Kama wamenitesa mimi na ninyi pia watawatesa; kama wamelishika neno langu na neno lenu watalishika pia. 21 Lakini yote haya watawatendea kwa ajili yangu kwa sababu hawamfahamu Baba yangu ambaye amenituma. 22 Kama sikuja na kusema nao wasingalikuwa na hatia. Lakini sasa hawana udhuru kwa dhambi zao. 23 Mtu ye yote anayenichukia mimi anamchukia na Baba yangu. 24 Kama nilikuwa sikuwafanyia miujiza ambayo haijapata kufanywa na mtu mwingine ye yote, wasingalikuwa na hatia ya dhambi. Lakini wameona miujiza hii na bado wakatuchukia mimi na Baba yangu. 25 “Hali hii imetokea kama ilivyoandikwa katika Sheria kwamba, ‘Walinichukia pasipo sababu.’

Kazi ya Roho Mtakatifu

26 Lakini atakapokuja yule Msaidizi nitakayewapelekea kutoka kwa Baba, yaani yule Roho wa kweli atokaye kwa Baba, yeye atanishuhudia mimi. 27 Na ninyi pia ni mashahidi wangu kwa maana tangu mwanzo mmekuwa pamoja nami.”

16 “Nimewaambia mambo haya yote ili msije mkapoteza imani yenu. Watawatenga na kuwatoa katika ushirika wa masinagogi. Na si hivyo tu, bali utafika wakati ambapo mtu ye yote atakayewaua atadhani kuwa anamtumikia Mungu. Watu watawatendea haya kwa sababu hawamfahamu Baba wala hawanifahamu mimi. Lakini nimew aambia mambo haya kusudi muda huo utakapofika mkumbuke kuwa nili kuwa nimewaambia. Sikuwaambia mambo haya tangu mwanzo kwa sababu nilikuwa pamoja nanyi. “Lakini sasa ninakwenda kwake yeye aliyenituma, wala hakuna mmoja wenu anayeniuliza, ‘Unakwenda wapi?’ Kwa kuwa nimewaambia mambo haya, mioyo yenu imejawa na huzuni. Lakini nawaambia kweli kwamba kuondoka kwangu ni kwa faida yenu kwa maana nisipoondoka, yule Msaidizi hatakuja kwenu. Lakini nikienda nitamtuma aje kwenu. Naye akija atauthibitishia ulim wengu kuhusu dhambi, haki na hukumu. Kuhusu dhambi kwa sababu hawaniamini; 10 kuhusu haki kwa sababu ninakwenda kwa Baba na hamtaniona tena; 11 na kuhusu hukumu kwa sababu mtawala wa ulim wengu huu amekwisha kuhukumiwa.

12 “Nina mambo mengi zaidi ya kuwaambia lakini hamwezi kuy apokea sasa. 13 Akija yule Roho wa kweli atawaongoza muijue kweli yote. Yeye hatanena kwa uwezo wake mwenyewe bali atanena yote atakayosikia. Atawafundisha kuhusu mambo yote yajayo. 14 Atanitukuza mimi, kwa maana atayachukua yaliyo yangu na kuwaambia ninyi. 15 Vyote alivyo navyo Baba ni vyangu, ndio maana nimesema kuwa atachukua yaliyo yangu na kuwaambia ninyi.

Huzuni ya Wanafunzi Itageuka Kuwa Furaha

16 “Baada ya muda mfupi hamtaniona tena; na kisha muda mfupi baadaye mtaniona.” 

17 Baadhi ya wanafunzi wakaulizana, “Ana maana gani asemapo, ‘Baada ya muda mfupi hamtaniona tena na muda mfupi baadaye mtaniona’? Na ana maana gani asemapo, ‘Kwa sababu ninakwenda kwa baba’?” 18 Wakaendelea kuulizana, “Ana maana gani asemapo, ‘muda mfupi?’ Hatuelewi ana maana gani!”

19 Yesu alitambua walilotaka kumwuliza kwa hiyo akawaambia, “Mnaulizana nina maana gani nisemapo, ‘Baada ya muda mfupi ham taniona tena na baada ya muda mfupi mtaniona?’ 20 Ninawaambia yaliyo hakika kwamba mtalia na kuomboleza lakini ulimwengu utafu rahi. Mtahuzunika lakini huzuni yenu itageuka kuwa furaha. 21 Mwanamke akaribiapo kuzaa huwa na huzuni kwa sababu saa yake ya uchungu imefika. Lakini mtoto azaliwapo mama anasahau mateso hayo kwa sababu ya furaha ya kuzaliwa mtoto duniani. 22 Na ninyi sasa mna huzuni lakini nitawaona tena na mtafurahi, wala hakuna atakayewaondolea furaha yenu. 23 Wakati huo hamtaniomba kitu cho chote. Ninawaambia kweli kwamba Baba yangu atawapa lo lote mta kaloomba kwa jina langu. 24 Mpaka sasa hamjaomba lo lote kwa jina langu. Ombeni nanyi mtapewa ili furaha yenu ipate kukamil ika.

25 “Nimewaambia mambo haya kwa mafumbo. Lakini wakati unakuja ambapo sitazungumza nanyi tena kwa mafumbo bali nita waeleza wazi wazi kuhusu Baba yangu. 26 Wakati huo mtaomba kwa jina langu. Wala sisemi kwamba nitamwomba Baba kwa niaba yenu; 27 kwa maana Baba mwenyewe anawapenda kwa sababu mmenipenda mimi na mmeamini kwamba nimetoka kwa Baba. 28 Nilitoka kwa Baba na nimekuja ulimwenguni, tena sasa naondoka ulimwenguni na ninak wenda kwa Baba.”

29 Wanafunzi wake wakasema, “Sasa unazungumza wazi wazi wala si kwa mafumbo. 30 Sasa tumejua kwamba wewe una jua mambo yote wala hakuna haja ya mtu kukuuliza maswali. Kwa hiyo tunaamini kwamba ulitoka kwa Mungu.”

31 Yesu akawajibu, “Sasa mnaamini? 32 Saa inakuja, tena imeshawadia, ambapo mtata wanyika, kila mtu aende nyumbani kwake na kuniacha peke yangu; lakini mimi siko peke yangu kwa sababu Baba yuko pamoja nami.

33 Nimewaambia mambo haya ili mpate kuwa na amani mkiwa ndani yangu. Ulimwenguni mtapata dhiki lakini jipeni moyo, kwa maana mimi nimeushinda ulimwengu.”