Skip to content

Utangulizi wa Mahubiri ya Mlimani

5 Yesu alipoona umati wa watu, alipanda mlimani akaketi chini. Wanafunzi wake wakamjia, naye akaanza kuwafundisha,

Vipimo

akisema:

“Wamebarikiwa walio maskini wa roho; maana Ufalme wa mbin guni ni wao. 

Wamebarikiwa wanaoomboleza; maana watafarijiwa. 

Wamebarikiwa walio wapole; maana watairithi nchi. 

Wamebari kiwa wenye hamu ya kutenda haki; maana wataridhishwa. 

Wamebari kiwa walio na huruma; maana nao watahurumiwa. 

Wamebarikiwa walio na moyo safi; maana watamwona Mungu. 

Wamebarikiwa walio wapatanishi; maana wataitwa wana wa Mungu. 

10 Wamebarikiwa wanaoteswa kwa kutenda haki; maana Ufalme wa mbinguni ni wao.

11 Mmebarikiwa ninyi wakati watu watakapowatukana na kuwatesa na kuwasingizia maovu kwa ajili yangu. 12 Shangilieni na kufurahi, kwa maana zawadi yenu huko mbinguni ni kubwa; kwa kuwa ndivyo walivyowatesa manabii waliowatangulia ninyi.

Chumvi na Mwanga

13 “Ninyi ni chumvi ya ulimwengu. Lakini chumvi ikipoteza ladha yake, haiwezekani kuwa chumvi tena. Haifai kwa kitu cho chote, ila kutupwa nje ikanyagwe na watu.

14 “Ninyi ni nuru ya ulimwengu. Mji uliojengwa kwenye mlima haufichiki. 15 Wala hakuna mtu anayewasha taa kisha akaifunika. Badala yake, huiweka mahali pa juu ili itoe mwanga kwa kila mtu aliyemo ndani ya nyumba. 16 Hali kadhalika, nuru yenu iwaangazie watu ili waone matendo yenu mema wamtukuze Baba yenu aliye mbin guni.’

Utimilifu wa Sheria

17 “Msidhani kwamba nimekuja kufuta sheria ya Musa na mafundisho ya manabii. kwamba mpaka mbingu na dunia zitaka potoweka, hakuna hata herufi moja ya sheria itakayopotea mpaka shabaha yake ikamilike. 19 Kwa hiyo ye yote atakayelegeza hata mojawapo ya amri ndogo kuliko amri zote na akawafundisha wengine kufanya hivyo, ataitwa mdogo kabisa katika Ufalme wa mbinguni. Sikuja kuzifuta bali kuzitimiza. 18 Kwa maana ninawaambia hakika Lakini atakayetii amri hizi na kuwafundisha wengine kuzitii a taitwa mkuu katika Ufalme wa mbinguni. 20 Kwa maana nawaambieni, ikiwa haki yenu haitazidi haki ya waandishi wa sheria na Mafari sayo, hamtaingia katika Ufalme wa mbinguni kamwe.”

Mauaji

21 “Mmesikia walivyowafundisha watu wa zamani kwamba, ‘Usiue; na ye yote atakayeua atastahili hukumu.’ 22 Lakini mimi nawaambia kwamba, ye yote atakayemkasirikia ndugu yake atasta hili hukumu; na ye yote atakayemtukana ndugu yake, atashtakiwa katika baraza; na ye yote atakayemwambia ndugu yake, ‘Wewe mjinga,’ atastahili hukumu ya moto wa Jehena.

23 “Basi, kama ulikuwa tayari kutoa sadaka yako madhaba huni, ukakumbuka kuwa ndugu yako amekukasirikia, 24 acha sadaka yako hapo hapo, uende kwanza ukapatane naye, kisha urudi kumtolea Mungu sadaka yako.

25 “Mtu akikushtaki, patana naye kabla hamjafika mahaka mani; ili mshtaki wako asije akakukabidhi kwa hakimu, na hakimu akamwamuru askari akufunge gerezani; 26 nami nawaambia hakika, hutatoka huko mpaka deni lako lote litakapolipwa.”

Uzinzi

27 “Mmesikia walivyowafundisha watu wa zamani kwamba, ‘Usi zini’. 28 Lakini mimi nawaambia: ye yote atakayemwangalia mwa namke kwa kumtamani, amekwisha kuzini naye moyoni mwake. 29 Jicho lako la kulia likikufanya utende dhambi, ling’oe ulitu pilie mbali. Ni afadhali upoteze sehemu ya mwili wako kuliko mwili mzima utupwe Jehena. 30 Na kama mkono wako wa kuume ukiku fanya utende dhambi, ukate uutupilie mbali. Ni afadhali upoteze sehemu ya mwili wako kuliko mwili mzima utupwe Jehena.

Talaka

31 “Pia mliambiwa kwamba, ‘Mtu ye yote anayemwacha mkewe ampe talaka.’ 32 Lakini mimi nawaambia, ye yote atakayempa mkewe talaka isipokuwa kwa kosa la uasherati, anamfanya mkewe mzinzi. Na ye yote atakayemwoa mwanamke aliyepewa talaka anazini.”

Viapo

33 “Tena mmesikia watu wa kale waliambiwa kwamba, ‘Usi vunje kiapo chako bali umtimizie Mungu kama ulivyoapa kutenda.’ 34 Lakini mimi nawaambia, msiape kabisa, ama kwa mbingu, kwa sababu ni kiti cha enzi cha Mungu, 35 au kwa ardhi, kwa sababu ndipo mahali pake pa kuwekea miguu, au kwa Yerusalemu kwa sababu ndio mji wa Mfalme mkuu. 36 Na msiape kwa vichwa vyenu kwa sababu hamwezi kugeuza hata unywele mmoja kuwa mweupe au mweusi. 37 Ukisema ‘Ndio’ basi iwe ‘Ndio’; na ukisema ‘Hapana’ basi iwe ‘ Hapana.’ Lo lote zaidi ya haya hutoka kwa yule mwovu.”

Jicho kwa Jicho

38 “Mmesikia kuwa watu zamani walikuwa wakisema, ‘Jicho kwa jicho na jino kwa jino.’ 39 Lakini mimi nawaambia, msishindane na mtu mwovu. Lakini mtu akikupiga kwenye shavu la kulia, mgeuzie na shavu la kushoto pia; 40 na kama mtu akitaka kukushtaki achukue shati lako, mwachie achukue na koti pia. 41 Na kama mtu akikulazimisha uende kilometa moja naye, fanya zaidi, nenda naye kilometa mbili. 42 Mtu akikuomba kitu mpe, na usikatae kumsaidia mtu anayetaka kukukopa.”

Upendo kwa Maadui

43 “Mmesikia kuwa watu zamani walikuwa wakisema, ‘Umpende jirani yako na umchukie adui yako.’ 44 Lakini mimi ninawaambia, wapendeni maadui zenu na waombeeni wanaowatesa, 45 ili mpate kuwa watoto wa Baba yenu aliye mbinguni. Kwa maana yeye huwaanga zia jua lake watu waovu na watu wema; na pia huleta mvua kwa wenye haki na wasio haki. 46 Kama mkiwapenda wanaowapenda tu, mtapata thawabu gani? Hata wenye dhambi hufanyiana hivyo. 47 Na kama mkiwasalimu ndugu zenu tu, mnafanya nini zaidi ya wengine? Hata watu wa mataifa wasiomjua Mungu, hufanya hivyo. 48 Kwa hiyo inawapasa ninyi muwe wakamilifu kama Baba yenu wa mbinguni alivyo mkamilifu.”

Kutoa kwa Wahitaji

6 “Angalieni msitende mema mbele ya watu ili muonekane na watu. Kwa maana mkifanya hivyo hamtapata thawabu itokayo kwa Baba yenu aliye mbinguni.

“Kwa hiyo mnapowasaidia maskini msitangaze kwa tarumbeta kama wafanyavyo wanafiki katika masinagogi na mitaani ili wasi fiwe na watu. Nawaambia wazi, wao wamekwisha pata tuzo yao. Lakini ninyi mnapotoa sadaka, fanyeni kwa siri, hata mkono wako wa kushoto usijue mkono wako wa kulia unafanya nini; ili sadaka yako iwe ni siri. Naye Baba yako wa mbinguni anayeona sirini ata kupa thawabu.”

Maombi

“Na mnaposali, msiwe kama wanafiki; maana wao wanapenda kusimama na kusali katika masinagogi na kando ya barabara ili waonekane na watu. Nawaambieni kweli, wao wamekwisha kupata tuzo yao. Unaposali, nenda chumbani kwako ufunge mlango na umwombe Baba yako aliye sirini. Na Baba yako aonaye sirini atakupa tha wabu. “Mnaposali msirudie maneno yale yale kama wafanyavyo watu wa mataifa wasiomjua Mungu. Kwa maana wao hudhani kwamba watasi kilizwa kwa sababu ya wingi wa maneno yao. Msiwe kama wao, kwa sababu Baba yenu anajua mahitaji yenu hata kabla hamjaomba.”

Basi msalipo ombeni hivi:

‘Baba yetu uliye mbinguni
jina lako litukuzwe.
10 Ufalme wako uje,
mapenzi yako yafanyike
hapa duniani kama huko mbinguni.
11 Utupatie leo riziki yetu ya kila siku.
12 Na utusamehe makosa yetu
     kama sisi tulivyokwisha kuwa samehe waliotukosea.
13 Na usitutie majaribuni,
     bali utuokoe kutokana na yule mwovu.

14 Kama mkiwasamehe watu makosa yao, Baba yenu wa mbinguni atawasamehe na ninyi; 15 lakini msipowasamehe watu makosa yao, Baba yenu hatawasamehe makosa yenu.

Kufunga

16 “Mnapofunga, msionyeshe huzuni kama wafanyavyo wanafiki. Maana wao hukunja nyuso zao ili kujionyesha. Nawaambieni kweli kwamba wao wamekwisha kupata tuzo yao. 17 Lakini mnapofunga, jipakeni mafuta kichwani na kuosha nyuso zenu 18 ili kufunga kwenu kusijulikane kwa mtu ila Baba yenu aliye sirini; na Baba yenu aonaye katika siri atawapa thawabu.” Akiba Ya Mbinguni.

Hazina Mbinguni

19 “Msijiwekee mali nyingi duniani ambapo wadudu na kutu huharibu na wezi huvunja na kuiba. 20 Lakini jiwekeeni mali mbinguni ambapo wadudu na kutu hawaharibu na wezi hawavunji na kuiba. 21 Kwa sababu pale akiba yako ilipo ndipo moyo wako uta kapokuwa.”

22 “Jicho ni taa ya mwili. Kama jicho lako ni zuri, mwili wako wote utakuwa na nuru. 23 Lakini kama jicho lako ni bovu, mwili wako wote utakuwa na giza. Kwa hiyo kama nuru iliyomo ndani yako ni giza, hakika utakuwa na giza la kutisha.”

24 “Hakuna mtu anayeweza kuwatumikia mabwana wawili, kwa sababu, ama atamchukia mmoja na kumpenda mwingine, au atamthami ni mmoja na kumdharau mwingine. Huwezi kumtumikia Mungu na mali.”

Usijali

25 “Kwa hiyo nawaambia, msiwe na wasiwasi kuhusu maisha yenu: mtakula nini au mtakunywa nini; au kuhusu miili yenu: mvae nini. Kwani maisha si zaidi ya chakula? Na mwili zaidi ya mavazi? 26 Waangalieni ndege wa angani: wao hawapandi wala kuvuna wala kuweka cho chote ghalani. Lakini Baba yenu wa mbinguni anawali sha. Je ninyi, si wa thamani zaidi kuliko ndege? 27 Ni nani kati yenu ambaye kwa kujihangaisha kwake anaweza kujiongezea hata saa moja zaidi kwenye maisha yake?

28 “Na kwa nini mnahangaikia mavazi? Angalieni maua ya mwi tuni yanavyostawi. Hayafanyi kazi wala hayashoni nguo. 29 Lakini nawaambia, hata mfalme Sulemani katika ufahari wake wote hakuwahi kuvikwa kama mojawapo la maua hayo. 30 Lakini ikiwa Mungu anay avisha hivi maua ambayo leo yapo na kesho yanatupwa motoni, je, hatawavisha ninyi vizuri zaidi, enyi watu wenye imani haba? 31 Kwa hiyo msiwe na wasiwasi mkisema, ‘Tutakula nini?’ au ‘Tutakunywa nini?’ au ‘Tutavaa nini?’ 32 Mambo haya ndio yanay owahangaisha watu wa mataifa wasiomjua Mungu; na Baba yenu wa mbinguni anafahamu kwamba mnahitaji yote hayo. 33 Lakini uta futeni kwanza Ufalme wa mbinguni na haki yake, na haya yote mtaongezewa. 34 Kwa hiyo msihangaike kuhusu kesho, kwa sababu kesho itajihangaikia yenyewe. Kila siku ina shida zake za kutosha.”

Kuwahukumu Wengine

7 Usihukumu ili na wewe usihukumiwe. Kwa maana hukumu uta kayotamka juu ya wenzako ndio itakayotumiwa kukuhukumu, na kipimo utakachotoa ndicho utakachopokea.

Kwa nini unaangalia kijiti kidogo kilichomo katika jicho la ndugu yako na wala huoni pande la mti lililoko jichoni mwako? Au unawezaje kumwambia ndugu yako, ‘Hebu nikutoe uchafu jichoni mwako,’ wakati jichoni mwako mna pande kubwa? Mnafiki wewe! Toa kwanza pande lililoko jichoni mwako, ndipo utaweza kuona vema, upate kukitoa kipande kilichoko ndani ya jicho la ndugu yako.

“Msiwape mbwa vitu vitakatifu; na msitupe lulu zenu mbele ya nguruwe wasije wakazikanyaga kanyaga na halafu wawageukie na kuwashambulia.”

Uliza, Tafuta, Gonga

“Ombeni nanyi mtapewa. Tafuteni nanyi mtapata; bisheni hodi nanyi mtafunguliwa mlango. Kwa sababu kila aombaye hupewa; naye atafutaye hupata; na abishaye hodi atafunguliwa mlango.

“Au ni nani kati yenu ambaye kama mwanae akimwomba mkate atampa jiwe? 10 Au akimwomba samaki atampa nyoka? 11 Ikiwa ninyi mlio waovu mnafahamu jinsi ya kuwapa watoto wenu zawadi nzuri, ni mara ngapi zaidi Baba yenu wa mbinguni atawapa vitu vizuri wale wamwombao? 12 Kwa hiyo cho chote ambacho ungependa watu wakutendee, na wewe watendee vivyo hivyo. Hii ndio maana ya sheria ya Musa na Maandiko ya manabii.”

Milango Nyembamba na Mipana

13 “Ingieni kwa kupitia mlango mwembamba; kwa maana mlango mpana na njia rahisi huelekea kwenye maangamizo, na watu wanaopitia huko ni wengi. 14 Lakini mlango mwembamba na njia ngumu huelekea kwenye uzima, na ni wachache tu wanaoiona.”

Manabii wa Kweli na wa Uongo

15 “Jihadharini na manabii wa uongo wanaowajia wakiwa wamevaa ngozi ya kondoo, kumbe ndani ni mbwa mwitu wakali. 16 Mtawatambua kwa matunda yao. Je, unaweza kuchuma zabibu kwenye miiba au tini kwenye michongoma? 17 Vivyo hivyo mti mzuri huzaa matunda mazuri na mti mbaya huzaa matunda mabaya. 18 Mti mzuri hauwezi kuzaa matunda mabaya na mti mbaya hauwezi kuzaa matunda mazuri. 19 Kila mti usiozaa matunda mazuri hukatwa katwa na kutupwa motoni. 20 Hivyo, mtawatambua kwa matunda yao.”

Wanafunzi wa Kweli na wa Uongo

21 “Si kila mtu anayesema, ‘Bwana, Bwana,’ ambaye ataingia katika Ufalme wa mbinguni ila ni wale wanaofanya mapenzi ya Baba yangu aliye mbinguni. 22 Siku ile itakapofika wengi wata niambia, ‘Bwana, Bwana, hatukutoa unabii na kufukuza pepo kwa jina lako; na kufanya miujiza mingi ya ajabu kwa jina lako?’ 23 Ndipo nitawaambia wazi, ‘Sikuwafahamu kamwe. Ondokeni kwangu ninyi watenda maovu!’

Wajenzi Wenye Busara na Wapumbavu

24 “Basi, kila anayesikiliza haya maneno yangu na kuyate keleza, atafanana na mtu mwenye busara aliyejenga nyumba yake kwenye mwamba. 25 Mvua ikanyesha, mafuriko yakaja na upepo uka vuma ukaipiga nyumba hiyo, lakini haikuanguka kwa sababu ili jengwa kwenye msingi imara juu ya mwamba. 26 Na kila anayesikia haya maneno yangu asiyafuate, atafanana na mtu mjinga aliyejenga nyumba yake kwenye mchanga. 27 Mvua ikanyesha, yakatokea mafu riko, na upepo ukavuma ukaipiga hiyo nyumba, nayo ikaanguka kwa kishindo kikubwa.”

28 Na Yesu alipomaliza kusema maneno haya, umati wa watu waliomsikiliza walishangaa sana, 29 kwa sababu alifundisha kama mtu mwenye mamlaka, na si kama walimu wao wa sheria.