Skip to content

Mzabibu umesinyaa, mtini nao umevia;
    Nao mkomamanga na mtende na mtofaa;
Naam, miti yote ya mashamba imekauka;
    Maana furaha imekauka katika wanadamu.

Yoeli 1:12

 “Nami nimewapiga kwa ukavu na koga; 
    wingi wa bustani zenu na mashamba yenu ya mizabibu,
na mitini yenu na mizeituni yenu imeliwa na tunutu;
    Lakini hamkunirudia mimi,”
    asema Bwana.

Amosi 4:9

Je! Mbegu ingali ghalani? Naam, huo mzabibu, wala mtini, wala mkomamanga, wala mzeituni, haikuzaa kitu; tangu siku hii ya leo nitawabariki.

Hagai 2:19

Na jeshi lote la mbinguni litafumuliwa, na mbingu zitakunjwa kama karatasi, na jeshi lao lote litanyauka kama vile jani la mzabibu linyaukavyo na kupukutika, na kama jani la mtini linyaukavyo na kupukutika.

Isaya 34:4

 Nitawaangamiza kabisa, asema Bwana; hapana zabibu katika mizabibu, wala tini katika mitini, hata jani lake litanyauka; na vitu vile nilivyowapa vitawapotea.

Yeremia 8:13