Mfano wa Wanawali Kumi
25 Mmoja alimpa talanta tano za fedha, mwingine mbili na mwingine moja; kila mmoja alipewa kwa kadiri ya uwezo wake. Kisha akasa firi. 2 Watano walikuwa wajinga na watano walikuwa na busara. 3 Wale wajinga walichukua taa zao bila akiba ya mafuta; 4 lakini wale wenye busara walichukua taa na mafuta ya akiba. 5 Bwana harusi alipoka wia wale wasichana wote walisinzia, wakalala.
6 Usiku wa manane zikapigwa kelele: ‘Bwana harusi anakuja! Tokeni nje kumlaki!’
7 Wasichana wote wakaamka, wakazitengeneza taa zao. 8 Wale wajinga wakawaambia wale wenye busara, ‘Tupatieni mafuta kidogo, taa zetu zinazimika.’
9 Lakini wenye busara wakajibu, ‘Pengine hayatatutosha sisi na ninyi pia, afadhali nendeni kwa wauza mafuta mkajinunulie wenyewe.’
10 Na walipokuwa wamekwenda kunu nua mafuta, bwana harusi akafika. Wale wasichana waliokuwa tayari wakaingia pamoja naye kwenye karamu ya harusi na mlango uka fungwa.
11 Baadaye wale wasichana wengine pia wakaja, wakaita, ‘Bwana! Bwana! Tufungulie mlango!’
12 Bwana harusi akawajibu, ‘Nawaambieni kweli, siwajui.’
13 Kwa hiyo kesheni, kwa sababu hamjui siku wala saa”
Mfano wa Mifuko ya Dhahabu
14 “Pia Ufalme wa mbinguni utafananishwa na mtu aliyekuwa anasafiri, akawaita watumishi wake na kuwakabidhi mali yake. 16 “Yule aliyepewa talanta tano alikwenda mara moja kuzifa nyia biashara akapata talanta tano zaidi. 17 Yule aliyepewa tal anta mbili akafanya hivyo hivyo, akapata mbili zaidi. 18 Lakini yule mtumishi aliyepata talanta moja, alikwenda akachimba shimo akaifukia huko.
19 “Baada ya muda mrefu yule bwana wa hao watumishi alirudi akakagua hesabu za fedha zake alizowaachia. 20 Yule mtumishi aliyepokea talanta tano akaja, akaleta talanta tano zaidi. Akasema, ‘Bwana ulinikabidhi talanta tano, hizi hapa, nimezalisha talanta tano zaidi.’
21 Bwana wake akamwambia, ‘Umefanya vizuri sana, mtumishi mwema na mwaminifu; umekuwa mwaminifu katika machache; nitakupa mamlaka juu ya vitu vingi zaidi. Njoo ufurahi pamoja na bwana wako.’
22 Yule mwenye talanta mbili naye akaja. Akasema, ‘Bwana, ulinikabidhi talanta mbili. Nami nimepata faida, hizi hapa talanta mbili zaidi.’
23 Bwana wake akajibu, ‘Umefanya vizuri sana, mtumishi mwema na mwaminifu; umekuwa mwaminifu katika machache, nami nitakupa mamlaka juu ya vitu vingi zaidi. Njoo ufurahi pamoja na bwana wako.’
24 Kisha yule mtumishi aliyepokea talanta moja akaja, akasema, ‘Bwana, nilijua kwamba wewe ni mtu mgumu, unavuna ambapo hukupanda na kukusanya ambapo hukutawanya mbegu. 25 Kwa hiyo niliogopa, nikaenda nikaificha talanta yako ardhini. Hii hapa mali yako.’
26 Lakini Bwana wake akamjibu, ‘Wewe mtumishi mwovu na mvivu! Ulijua kwamba ninavuna nisipopanda na kukusanya nisipota wanya mbegu? 27 Mbona basi hukuweka fedha zangu benki ili nita kaporudi nizichukue na faida yake?
28 Mnyang’anyeni hiyo talanta mumpatie yule mwenye talanta kumi.’ 29 Kwa maana kila mtu mwenye kitu ataongezewa, naye atakuwa navyo kwa wingi. Lakini kwa yule asiye na kitu, hata kidogo alicho nacho atanyang’anywa. 30 ‘Mtupeni huyo mtumishi asiyefaa nje kwenye giza, huko kuta kuwa na kilio na kusaga meno.’ ”
Kondoo na Mbuzi
31 “Mwana wa Adamu atakapokuja katika utukufu wake pamoja na malaika wote, ataketi katika kiti chake cha utukufu cha enzi. 32 Watu wa mataifa yote watakusanyika mbele yake, naye atawaten ganisha kama mchungaji anavyotenganisha kondoo na mbuzi. 33 Atawaweka kondoo upande wa kulia na mbuzi upande wa kushoto.
34 Ndipo Mfalme atawaambia wale walioko upande wa kulia, ‘Njooni ninyi mliobarikiwa na Baba yangu, urithini Ufalme mlioandaliwa tangu mwanzo wa dunia. 35 Kwa maana nilikuwa na njaa mkanipa chakula; nilikuwa na kiu mkanipa kitu cha kunywa; nilikuwa mgeni mkanikaribisha; 36 nilikuwa sina nguo, mkanivisha; nilikuwa mgonjwa mkaja kunitazama; na nilikuwa kifungoni mkaja kunitembe lea.’
37 “Kisha wale wenye haki watamjibu, ‘Bwana, ni lini tuli kuona na njaa tukakulisha au ukiwa na kiu tukakupa kitu cha kunywa ? 38 Na ni lini tulikuona ukiwa mgeni tukakukaribisha au ukihitaji nguo tukakuvisha? 39 Na ni lini tulikuona ukiwa mgonjwa au ukiwa kifungoni tukakutembelea?’
40 “Mfalme atajibu, ‘Ninawaambia kweli, kwa jinsi ambavyo mlivyomfanyia mmojawapo wa hawa ndugu zangu walio wadogo, mlini fanyia mimi.’
41 “Kisha atawaambia wale walio kushoto kwake, ‘Ondokeni kwangu ninyi mliolaaniwa, nendeni katika moto wa milele alioan daliwa shetani na malaika zake. 42 Kwa maana nilikuwa na njaa hamkunipa chakula; nilikuwa na kiu na hamkunipa kitu cha kunywa; 43 nilikuwa mgeni wala hamkunikaribisha; nilikuwa uchi hamkuni vika; na nilikuwa mgonjwa na gerezani nanyi hamkuja kunitazama.’
44 “Ndipo wao pia watajibu, ‘Bwana ni lini tulikuona ukiwa na njaa au kiu, au ukiwa mgeni au ukihitaji nguo, au ukiwa mgonjwa na kifungoni na hatukukuhudumia?’
45 “Naye atawajibu, ‘Nawaambieni kweli, kwa jinsi ambavyo hamkumfanyia mmojawapo wa hawa ndugu zangu walio wadogo, hamkuni fanyia mimi.’
46 “Basi hawa wataingia katika adhabu ya milele, lakini wale wenye haki wataingia katika uzima wa milele.”