Skip to content

From the Books

Katika Wiki ya kwanza

Jumapili hiyo jioni, wakati wanafunzi walikuwa pamoja huku milango ikiwa imefungwa kwa kuwaogopa Wayahudi, Yesu aliwato kea! Akasimama kati yao akasema, “Amani iwe nanyi.” 20 Baada ya kusema haya, aliwaonyesha mikono yake na ubavu wake. Wanafunzi walifurahi sana walipomwona Bwana!

21 Yesu akawaambia tena, “Amani iwe nanyi. Kama Baba alivyonituma, mimi pia nawatuma ninyi.” 22 Na alipokwisha kusema haya akawavuvia pumzi yake akawaambia, “Pokeeni Roho Mtakatifu. 23 Mkimsamehe mtu ye yote dhambi zake, atakuwa amesamehewa. Msipomsamehe, atakuwa hajasame hewa.”

Yesu Anamtokea Tomaso

24 Tomaso, aliyeitwa Pacha, hakuwepo wakati Yesu aliwatokea wanafunzi wenzake. 25 Kwa hiyo wakamwambia, “Tumemwona Bwana.”

Lakini yeye akawaambia, “Sitaamini mpaka nione alama za misumari katika mikono yake na niguse kwa vidole vyangu makovu ya misumari na kuweka mkono wangu ubavuni mwake.”

26 Siku nane baada ya haya, wanafunzi walikuwa pamoja tena katika chumba kimoja na Tomaso pia alikuwepo. Milango ilikuwa imefungwa, lakini Yesu akawatokea akasimama kati yao akawaambia, “Amani iwe nanyi.” 27 Ndipo akamwambia Tomaso, “Weka kidole chako hapa; tazama mikono yangu halafu nyoosha mkono wako uguse ubavu wangu. Usiwe na mashaka bali uamini.”

28 Tomaso akasema, “Bwana wangu na Mungu wangu!” God!”

29 Yesu akamwambia, “Umeamini kwa kuwa umeniona? Wamebarikiwa wale ambao hawajaona lakini wameamini.”

Kusudi la Injili ya Yohana

30 Yesu alifanya ishara nyingine nyingi mbele za wanafunzi wake ambazo hazikuandikwa katika kitabu hiki. 31 Lakini hizi zimeandikwa ili muweze kuamini ya kuwa Yesu ndiye Kristo, Mwana wa Mungu; na kwa kumwamini mpate uzima katika jina lake.

Yohana 20:19-31

Baada ya Wiki ya Kwanza

Baada ya haya Yesu alijitambulisha tena kwa wanafunzi wake kando ya bahari ya Tiberia. Ilitokea hivi: Simoni Petro, Tomaso aitwaye Pacha, Nathanaeli wa Kana ya Galilaya, wana wa Zebedayo na wanafunzi wengine wawili walikuwa pamoja. Simoni Petro aka waambia wenzake, “Mimi nakwenda kuvua samaki.” Nao wakamwambia, “Tutakwenda pamoja nawe.” Wakatoka, wakaingia ndani ya mashua. Lakini usiku ule hawakupata cho chote.

 Kulipopambazuka, Yesu alisimama ufukoni, lakini wale wana funzi hawakumtambua.

Yesu akawaambia, “Wanangu, mmepata samaki wo wote?”

Wakamjibu, “La.”

Akawaambia, “Shusheni wavu upande wa kulia wa mashua yenu nanyi mtapata samaki.” Walivyofa nya hivyo walipata samaki wengi mno hata wakashindwa kuingiza ule wavu uliojaa samaki katika mashua! 

Kisha yule mwanafunzi ali yependwa na Yesu akamwambia Petro, “Ni Bwana!” Petro aliposikia haya akajifunga nguo yake, kwa kuwa alikuwa amevua wakati wakifa nya kazi, akajitosa baharini, akaogelea kuelekea ufukoni. Wale wanafunzi wengine wakaja kwa ile mashua huku wakivuta ule wavu uliojaa samaki. Hapo walipokuwa wakivua hapakuwa mbali na nchi kavu; ilikuwa kama hatua mia moja hivi. Walipowasili nchi kavu, wakaona moto wa mkaa na samaki wakiokwa juu yake, na mikate.

10 Yesu akawaambia, “Leteni baadhi ya samaki mliovua.” 11 Simoni Petro akaenda akauvuta ule wavu ambao ulikuwa umejaa samaki wakubwa mia moja hamsini na tatu, akauleta ufukoni. Ingawa samaki walikuwa wengi kiasi hicho, ule wavu haukuchanika. 12 Yesu akawaambia, “Njooni mle.” Hakuna hata mmoja wao aliyethubutu kumwuliza, “Wewe ni nani?” Walijua hakika ya kuwa ni Bwana. 13 Yesu akaenda akachu kua ile mikate na baadaye samaki, akawagawia. 14 Hii ilikuwa ni mara ya tatu Yesu kujitambulisha kwa wanafunzi wake tangu afufuke kutoka kwa wafu.

Yesu Amrejesha Petro

15 Walipokwisha kula, Yesu akamwuliza Simoni Petro, “Simoni mwana wa Yohana, unanipenda kweli kuliko hawa?”

Yeye akamjibu, “Ndio Bwana, wewe unajua ya kuwa nakupenda.”

Yesu akamwambia, “Lisha wana kondoo wangu.”

16 Kwa mara nyingine Yesu akamwul iza Simoni Petro, “Simoni, mwana wa Yohana, unanipenda?”

Petro akajibu, “Ndio Bwana, wewe unajua ya kuwa nakupenda.”

Akamwambia, “Chunga kondoo wangu.”

17 Kwa mara ya tatu Yesu akamwul iza Petro, “Simoni mwana wa Yohana, unanipenda?”

Petro akahuzu nika sana kwa kuwa Yesu alimwuliza mara ya tatu, ‘Unanipenda?’ Akamjibu, “Bwana, wewe unajua kila kitu. Unajua ya kuwa naku penda.”

Yesu akamwambia, “Lisha kondoo wangu. 18 Nakuambia wazi, ulipokuwa kijana ulivaa na kwenda unakotaka; lakini ukiwa mzee utanyoosha mikono yako na mtu mwingine atakuvika nguo na kukupeleka usipotaka kwenda.” 19 Alisema haya ili kumfahamisha Petro jinsi atakavyokufa, na kwa kifo hicho Mungu atukuzwe. Kisha Yesu akamwambia Petro, “Nifuate.”

20 Petro akageuka akamwona yule mwanafunzi aliyependwa na Yesu akiwafuata. Huyu mwanafunzi ndiye yule aliyekaa karibu kabisa na Yesu alipokula naye chakula cha mwisho akauliza, ‘Bwana, ni nani atakayekusaliti?’ 21 Petro alipomwona huyo mwanafunzi akamwuliza Yesu, “Bwana, na huyu je?”

22 Yesu akamjibu, “ Ikiwa nataka aishi mpaka nitakapo rudi, inakuhusu nini? Wewe nifuate!” 23 Kwa sababu ya maneno haya ya Yesu, uvumi ukaenea kati ya ndugu kwamba huyu mwanafunzi hangekufa. Lakini Yesu hakusema kuwa hangekufa. Yeye alisema tu kwamba, “Ikiwa nataka aishi mpaka nitakaporudi, inakuhusu nini?”

24 Huyu ndiye yule mwanafunzi ambaye anashuhudia mambo haya na ndiye ambaye ameandika habari hizi. Nasi tunajua ya kuwa ushu huda wake ni wa kweli.

25 Yesu alifanya mambo mengine mengi pia. Ikiwa kila moja yao ingeandikwa, nadhani hata ulimwengu wote usingekuwa na nafasi ya vitabu ambavyo vingeandikwa

Yohana 21:1-25

Kuondoka Kwake Mbinguni

Mpendwa Teofilo, Katika Kitabu changu cha kwanza nilikuan dikia kuhusu mambo yote aliyotenda Yesu, hadi wakati alipopaa mbinguni. Kabla hajachukuliwa juu, aliwapa mitume wake maagizo kwa njia ya Roho Mtakatifu. Alijionyesha kwao akiwa hai muda wa siku arobaini baada ya kufufuka kwake. Akawahakikishia kwa njia nyingi ya kuwa ni yeye na akaongea nao kuhusu Ufalme wa Mungu. Wakati mmoja alipokuwa nao, aliwapa amri hii, “Msiondoke Yerusalemu, mpaka mtakapopokea ahadi aliyotoa Baba, ambayo mmeni sikia nikiizungumzia. Kwa maana Yohana aliwabatiza kwa maji lakini baada ya siku chache mtabatizwa kwa Roho Mtakatifu.”

Mitume walipokutana na Yesu walimwuliza, “Bwana, wakati huu ndipo utawarudishia Waisraeli ufalme?”

Yesu akawaambia, “Si juu yenu kufahamu wakati na majira ambayo yamewekwa na Baba kwa mamlaka yake. Lakini mtapokea nguvu akishawajilia Roho Mtakatifu, nanyi mtakuwa mashahidi wangu katika Yerusalemu na Yudea yote na Samaria, hadi mwisho wa dunia.”

Baada ya kusema haya, wakiwa wanatazama, alichukuliwa juu, na wingu likamficha wasimwone tena.

10 Walikuwa bado wakikaza macho yao mawinguni alipokuwa akienda, ndipo ghafla, wanaume wawili waliovaa mavazi meupe walisimama karibu nao, 11 wakasema, “Ninyi watu wa Galilaya, mbona mnasimama hapa mkitazama mbin guni? Yesu huyu huyu aliyechukuliwa mbinguni atarudi tena kama mlivyomwona akienda mbinguni.”

Matendo Ya Mitume 1:1-11

Mwanzo 1-2

Mwanzo

1 Hapo mwanzo Mungu aliziumba mbingu na nchi. Nayo nchi ilikuwa ukiwa, tena utupu, na giza lilikuwa juu ya uso wa vilindi vya maji; Roho ya Mungu ikatulia juu ya uso wa maji.

Mungu akasema, Iwe nuru; ikawa nuru. Mungu akaiona nuru, ya kuwa ni njema; Mungu akatenga nuru na giza. Mungu akaiita nuru Mchana, na giza akaliita Usiku. Ikawa jioni ikawa asubuhi, siku moja.

Mungu akasema, Na liwe anga katikati ya maji, likayatenge maji na maji. Mungu akalifanya anga, akayatenga yale maji yaliyo juu ya anga na yale maji yaliyo chini ya anga; ikawa hivyo. Mungu akaliita lile anga Mbingu. Ikawa jioni ikawa asubuhi, siku ya pili.

Mungu akasema, Maji yaliyo chini ya mbingu na yakusanyike mahali pamoja, ili pakavu paonekane; ikawa hivyo. 10 Mungu akapaita pale pakavu Nchi; na makusanyiko ya maji akayaita Bahari; Mungu akaona ya kuwa ni vyema.

11 Mungu akasema, Nchi na itoe majani, mche utoao mbegu, na mti wa matunda uzaao matunda kwa jinsi yake, ambao mbegu zake zimo ndani yake, juu ya nchi; ikawa hivyo. 12 Nchi ikatoa majani, mche utoao mbegu kwa jinsi yake, na mti uzaao matunda, ambao mbegu zake zimo ndani yake, kwa jinsi yake; Mungu akaona ya kuwa ni vyema. 13 Ikawa jioni ikawa asubuhi, siku ya tatu.

14 Mungu akasema, Na iwe mianga katika anga la mbingu ili itenge kati ya mchana na usiku; nayo iwe ndiyo dalili na majira na siku na miaka; 15 tena iwe ndiyo mianga katika anga la mbingu itie nuru juu ya nchi; ikawa hivyo. 16 Mungu akafanya mianga miwili mikubwa, ule mkubwa utawale mchana, na ule mdogo utawale usiku; akafanya na nyota pia. 17 Mungu akaiweka katika anga la mbingu, itie nuru juu ya nchi 18 na kuutawala mchana na usiku na kutenga nuru na giza; Mungu akaona ya kuwa ni vyema. 19 Ikawa jioni ikawa asubuhi, siku ya nne.

20 Mungu akasema, Maji na yajawe kwa wingi na kitu kiendacho chenye uhai, na ndege waruke juu ya nchi katika anga la mbingu. 21 Mungu akaumba nyangumi wakubwa, na kila kiumbe chenye uhai kiendacho, ambavyo maji yalijawa navyo kwa wingi kwa jinsi zao, na kila ndege arukaye, kwa jinsi yake; Mungu akaona ya kuwa ni vyema. 22 Mungu akavibarikia, akisema, Zaeni, mkaongezeke, mkayajaze maji ya baharini, ndege na wazidi katika nchi. 23 Ikawa jioni ikawa asubuhi, siku ya tano.

24 Mungu akasema, Nchi na izae kiumbe hai kwa jinsi zake, mnyama wa kufugwa, nacho kitambaacho, na wanyama wa mwitu kwa jinsi zake; ikawa hivyo. 25 Mungu akafanya mnyama wa mwitu kwa jinsi zake, na mnyama wa kufugwa kwa jinsi zake, na kila kitu kitambaacho juu ya nchi kwa jinsi yake; Mungu akaona ya kuwa ni vyema.

26 Mungu akasema, Na tumfanye mtu kwa mfano wetu, kwa sura yetu; wakatawale samaki wa baharini, na ndege wa angani, na wanyama, na nchi yote pia, na kila chenye kutambaa kitambaacho juu ya nchi.

27 Mungu akaumba mtu kwa mfano wake, kwa mfano wa Mungu alimwumba, mwanamume na mwanamke aliwaumba.

28 Mungu akawabarikia, Mungu akawaambia, Zaeni, mkaongezeke, mkaijaze nchi, na kuitiisha; mkatawale samaki wa baharini, na ndege wa angani, na kila kiumbe chenye uhai kiendacho juu ya nchi.

29 Mungu akasema, Tazama, nimewapa kila mche utoao mbegu, ulio juu ya uso wa nchi yote pia, na kila mti, ambao matunda yake yana mbegu; vitakuwa ndivyo chakula chenu; 30 na chakula cha kila mnyama wa nchi, na cha kila ndege wa angani, na cha kila kitu kitambaacho juu ya nchi, chenye uhai; majani yote ya miche, ndiyo chakula chenu; ikawa hivyo.

31 Mungu akaona kila kitu alichokifanya, na tazama, ni chema sana. Ikawa jioni ikawa asubuhi, siku ya sita.

2 Basi mbingu na nchi zikamalizika, na jeshi lake lote.

Na siku ya saba Mungu alimaliza kazi yake yote aliyoifanya; akastarehe siku ya saba, akaacha kufanya kazi yake yote aliyoifanya.

Adamu na Hawa

Hivyo ndivyo vizazi vya mbingu na nchi zilipoumbwa. Siku ile Bwana Mungu alipoziumba mbingu na nchi

hapakuwa na mche wa kondeni bado, wala mboga ya kondeni haijachipuka bado, kwa maana Bwana Mungu hajainyeshea nchi mvua, wala hapana mtu wa kuilima ardhi; ukungu ukapanda katika nchi, ukatia maji juu ya uso wote wa ardhi. Bwana Mungu akamfanya mtu kwa mavumbi ya ardhi, akampulizia puani pumzi ya uhai; mtu akawa nafsi hai.

Bwana Mungu akapanda bustani upande wa mashariki wa Edeni, akamweka ndani yake huyo mtu aliyemfanya. Bwana Mungu akachipusha katika ardhi kila mti unaotamanika kwa macho na kufaa kwa kuliwa; na mti wa uzima katikati ya bustani, na mti wa ujuzi wa mema na mabaya.

10 Ukatoka mto katika Edeni wa kuitilia bustani maji, na kutokea hapo ukagawanyika kuwa vichwa vinne. 11 Jina la wa kwanza ni Pishoni; ndio unaozunguka nchi yote ya Havila, ambako kuna dhahabu; 12 na dhahabu ya nchi ile ni njema; huko kuna bedola, na vito shoham. 13 Na jina la mto wa pili ni Gihoni; ndio unaozunguka nchi yote ya Kushi. 14 Na jina la mto wa tatu ni Hidekeli; ndio unaopita mbele ya Ashuru. Na mto wa nne ni Frati.

15 Bwana Mungu akamtwaa huyo mtu, akamweka katika bustani ya Edeni, ailime na kuitunza. 16 Bwana Mungu akamwagiza huyo mtu, akisema, Matunda ya kila mti wa bustani waweza kula, 17 walakini matunda ya mti wa ujuzi wa mema na mabaya usile, kwa maana siku utakapokula matunda ya mti huo utakufa hakika.

18 Bwana Mungu akasema, Si vema huyo mtu awe peke yake, nitamfanyia msaidizi wa kufanana naye.

19 Bwana Mungu akafanyiza kutoka katika ardhi kila mnyama wa msituni, na kila ndege wa angani, akamletea Adamu ili aone atawaitaje; kila kiumbe hai, jina alilokiita Adamu likawa ndilo jina lake. 20 Adamu akawapa majina yao kila mnyama wa kufugwa, na ndege wa angani, na kila mnyama wa mwituni;

lakini hakuonekana wa kumsaidia Adamu aliyefanana naye. 21 Bwana Mungu akamletea Adamu usingizi mzito, naye akalala; kisha akatwaa ubavu wake mmoja, akafunika nyama mahali pake, 22 na ule ubavu alioutwaa katika Adamu Bwana Mungu akaufanya mwanamke, akamleta kwa Adamu.

23 Adamu akasema,

Sasa huyu ni mfupa katika mifupa yangu, na nyama katika nyama yangu, basi ataitwa mwanamke, kwa maana ametwaliwa katika mwanamume.

24 Kwa hiyo mwanamume atamwacha baba yake na mama yake naye ataambatana na mkewe, nao watakuwa mwili mmoja.

25 Nao walikuwa uchi wote wawili, Adamu na mkewe, wala hawakuona haya.

Yesu Anaomba Atukuzwe

17 Yesu alipomaliza kusema maneno haya, alitazama mbinguni akasema,

“Baba, wakati umefika. Dhihirisha utukufu wangu ili nami nikutukuze wewe, kwa kuwa umenipa mamlaka juu ya watu wote, niwape uzima wa milele wale ambao umewakabidhi kwangu. Na huu ndio uzima wa milele: wakufahamu wewe ambaye pekee ni Mungu wa kweli, nakumfah amu Yesu Kristo ambaye umemtuma. Baba nime kutukuza hapa duniani kwa kutimiza kazi uliyonipa niifanye. Na sasa Baba nipe mbele yako ule utukufu niliokuwa nao pamoja na wewe hata kabla dunia haijaumbwa.

Yesu Anawaombea Wanafunzi Wake

Nimewafahamisha jina lako wale ambao umenipa kutoka katika ulimwengu. Wao wametii neno lako. Sasa wamefahamu ya kuwa vyote ulivyonipa vinatoka kwako ; kwa kuwa nimewapa ujumbe ulionipa, nao wameupokea. Wamefahamu hakika ya kuwa nimetoka kwako na wameamini kwamba ulinituma. Siwaombei watu wote wa ulimwengu bali nawaombea hawa ulionipa kwa sababu wao ni wako. 10 Wote ulionipa ni wako, na walio wako ni wangu; nao wanadhihirisha utukufu wangu. 11 Mimi naondoka ulimwenguni ninakuja kwako. Lakini wao wako ulimwenguni. Baba Mtakatifu, walinde kwa jina lako ambalo umenipa ili wawe na umoja kama sisi tulivyo mmoja. 12 Nilipokuwa pamoja nao niliwalinda wakawa salama kwa uwezo wa jina ulilonipa. Nimewalinda na hakuna hata mmoja aliyepotea, isipokuwa yule aliyeamua kupotea, ili Maandiko yapate kutimia.

13 Lakini sasa nakuja kwako na ninasema haya wakati nikiwa ulimwenguni, ili wawe na furaha yangu kikamil ifu. 14 Nimewapa neno lako na ulimwengu umewachukia kwa kuwa wao, kama mimi, si wa ulimwengu huu. 15 Siombi kwamba uwaondoe ulimwenguni, bali uwalinde na yule mwovu shetani. 16 Kama mimi nisivyo mwenyeji wa ulimwengu huu, wao pia sio wa ulimwengu. 17 Watakase kwa neno lako; kwa maana neno lako ndilo kweli. 18 Kama ulivyonituma mimi ulimwenguni, nami nawatuma wao ulim wenguni. 19 Kwa ajili yao nimejitoa wakfu kwako ili na wao wapate kuwa watakatifu kwa kufahamu kweli yako.

Yesu Anawaombea Waamini Wote

20 “Siwaombei hawa peke yao; bali nawaombea pia wale wote watakaoniamini kwa sababu ya ushuhuda wa hawa. 21 Ninawaombea wote wawe kitu kimoja kama vile wewe Baba ulivyo ndani yangu na mimi ni ndani yako; ili na wao wawe ndani yetu na ulimwengu upate kuamini ya kuwa wewe ulinituma. 22 Nimewapa utukufu ule ule ulionipa ili wawe kitu kimoja kama sisi tulivyo – 23 mimi nikiwa ndani yao na wewe ndani yangu; ili wakamilike katika umoja na ulimwengu upate kujua ya kuwa umenituma na kwamba unawapenda kama unavyonipenda mimi.

24 Baba, shauku yangu ni kwamba, hawa watu ulionipa wawepo mahali nilipo ili waweze kuona utukufu wangu; utukufu ambao umenipa kwa kuwa ulinipenda hata kabla ulimwengu haujaumbwa.

25 Baba Mtakatifu, ijapokuwa ulimwengu haukufahamu wewe, mimi ninakufahamu, na hawa wanajua ya kuwa umenituma. 26 Nimekutambulisha wewe kwao, na nitaendelea kulitambulisha jina lako kwao ili upendo ulio nao kwangu uwe upendo wao pia; nami niwe ndani yao.”

Yesu Anaosha Miguu ya Wanafunzi Wake

13 Ilikuwa siku moja kabla ya sikukuu ya Pasaka. Yesu alijua ya kuwa wakati wake wa kuondoka duniani na kurudi kwa Baba yake umekaribia. Alikuwa amewapenda sana wafuasi wake hapa duniani, akawapenda hadi mwisho.

Na wakati alipokuwa akila chakula cha jioni pamoja na wanafunzi wake, shetani alikuwa amekwisha kumpa Yuda Iskariote, mwana wa Simoni, wazo la kumsaliti Yesu. Yesu akijua ya kwamba Baba yake alikwisha mpa mamlaka juu ya vitu vyote; na kwamba yeye alitoka kwa Mungu na alikuwa anarudi kwa Mungu, alitoka mezani akaweka vazi lake kando, akajifunga taulo kiunoni. Kisha akamimina maji katika chombo akaanza kuwaosha wanafunzi wake miguu na kuikausha kwa ile taulo aliyojifunga kiu noni.

Alipomfikia Simoni Petro, Petro akamwambia, “Bwana, wewe unaniosha miguu?”

Yesu akamjibu, “Hivi sasa huelewi ninalofa nya lakini baadaye utaelewa.”

Petro akamjibu, “La, hutaosha miguu yangu kamwe!”

Yesu akamwambia, “Kama sitaosha miguu yako, huwezi kuwa mfuasi wangu.”

Ndipo Petro akasema, “Kama ni hivyo Bwana, nioshe miguu yangu pamoja na mikono yangu na kichwa changu pia!” 

10 Yesu akamwambia, “Mtu aliyekwishaoga ni safi mwili mzima naye hahitaji tena kunawa ila kuosha miguu tu. Ninyi nyote ni safi, isipokuwa mmoja.” 11 Yesu alifahamu ni nani angemsaliti, ndio sababu akasema, “Ninyi nyote ni safi, isipo kuwa mmoja.”

12 Alipomaliza kuwaosha miguu alivaa tena vazi lake, akarudi alipokuwa amekaa, ndipo akawaambia, “Je, mnaelewa maana ya jambo nililowafanyia? 13 Ninyi mnaniita mimi, Mwalimu na Bwana, na hii ni sawa, kwani ni kweli. 14 Kwa hiyo ikiwa mimi niliye Bwana wenu na Mwalimu wenu nimewaosha miguu, ninyi pia hamna budi kuoshana miguu. 15 Mimi nimewaonyesha mfano, ili mtendeane kama nilivyowafanyia. 16 Ninawaambia hakika, mtumishi hawezi kuwa mkuu kuliko bwana wake; wala anayetumwa hawezi kuwa mkuu kuliko aliyemtuma. 17 Kwa kuwa sasa mnafahamu mambo haya, mtabarikiwa na Mungu ikiwa mtayafanya.

Yesu Anatabiri Usaliti Wake

18 Siwazungumzii ninyi nyote. Ninawa fahamu wote niliowachagua. Maandiko yaliyotamka, ‘Yeye aliyekula chakula pamoja nami amekuwa msaliti wangu,’ hayana budi kutimia.

19 Ninawaambia mambo haya kabla hayajatokea ili yatakapotokea mpate kuamini ya kuwa mimi ndiye Kristo. 20 Nawahakikishia kuwa mtu anayemkubali na kumpokea ye yote ninayemtuma, ananipokea mimi. Na mtu anayenikubali na kunipokea, anampokea Baba yangu ambaye amenituma.”

21 Baada ya haya Yesu alifadhaika sana moyoni, akasema, “Ninawaambia wazi, mmoja wenu atanisaliti.”

22 Wanafunzi wake wakatazamana kwa wasiwasi, kwa kuwa hawakujua anamsema nani. 23 Mmoja wa wanafunzi ambaye Yesu alimpenda sana alikuwa amekaa karibu sana na Yesu. 24 Kwa hiyo Simoni Petro akamwashiria yule mwanafunzi akamwambia, “Tuambie, ni nani anayemsema.”

25 Yule mwanafunzi akimwegemea Yesu akamwambia, “Tafadhali Bwana tuambie, ni nani unayemzungumzia?”

26 Yesu akajibu, “Ni yule nitakayempa hiki kipande cha mkate baada ya kukichovya.” Kwa hiyo baada ya kuchovya ule mkate akampa Yuda, mwana wa Simoni Iskariote. 27 Mara tu baada ya kukipokea kile kipande cha mkate, shetani akamwingia moyoni.

Yesu akamwambia Yuda, “Jambo unalok wenda kufanya, kalifanye haraka.’ 28 Hakuna hata mmoja wa wale wengine waliokuwepo pale mezani aliyeelewa maana ya maneno aliy otamka Yesu. 29 Baadhi yao walidhani kwamba alikuwa anamwagiza akanunue vitu watakavyohitaji kwa ajili ya sikukuu au awape mas kini cho chote, kwa kuwa yeye alikuwa mtunza fedha. 30 Kwa hiyo mara baada ya kupokea ule mkate, Yuda alienda zake nje. Wakati huo giza lilikwisha ingia.

Yesu Anatabiri Kukana kwa Petro

31 Yuda alipokwisha ondoka, Yesu akawaambia, “Wakati ume karibia ambapo watu wataona utukufu wangu mimi Mwana wa Adamu na kwa njia hii watu watauona utukufu wa Mungu. 32 Na ikiwa Mungu atatukuzwa, yeye atanipa mimi utukufu wake, na atafanya hivyo mara.

33 Wapendwa wangu, muda wangu wa kuwa pamoja nanyi umekar ibia kwisha. Mtanitafuta; na kama nilivyowaambia Wayahudi, nina waambia na ninyi: ‘ninapokwenda hamwezi kunifuata’.

34 Nina waachia amri mpya: pendaneni ninyi kwa ninyi. Kama mimi nilivy owapenda, na ninyi mpendane vivyo hivyo. 35 Kama mkipendana hivyo, watu wote watafahamu ya kuwa ninyi ni wanafunzi wangu.”

36 Simoni Petro akamwuliza, “Bwana, kwani unakwenda wapi?”

Yesu akamjibu, “Ninapokwenda hamwezi kunifuata sasa, lakini mtanifuata baadaye.”

37 Petro akamwuliza tena, “Bwana, kwa nini siwezi kukufuata sasa? Mimi niko tayari kufa kwa ajili yako.”

38 Yesu akamjibu, “Je, ni kweli uko tayari kutoa maisha yako kwa ajili yangu? Ninakwambia hakika ya kuwa, kabla jogoo hajawika, utakanusha mara tatu kwamba hunijui.”

Yesu Awafariji Wanafunzi Wake

14 Yesu akawaambia, “Msifadhaike mioyoni mwenu. Mwaminini Mungu, niaminini na mimi pia. Katika nyumba ya baba yangu mna nafasi nyingi. Kama sivyo, nisingeliwaambia kwamba nakwenda kuwaandalia makao. Na nikishawaandalia, nitarudi kuwachukua mkae pamoja nami; ili mahali nilipo, nanyi mpate kuwepo. Ninyi mnajua njia ya kufikia ninakokwenda.”

Yesu Njia ya kwenda kwa Baba

Tomaso akamwuliza, “Bwana, hatujui unakokwenda; tutaijuaje njia?”

Yesu akawaam bia, “Mimi ndiye Njia na Kweli na Uzima; mtu hawezi kufika kwa Baba bila kupitia kwangu. Kama mngekuwa mnajua mimi ni nani, mngemfahamu na Baba yangu. Tangu sasa mnamfahamu Baba yangu na mmemwona.”

Filipo akamwambia Yesu, “Bwana, tuonyeshe Baba yako nasi tutaridhika.”

Yesu akamjibu, “Filipo, imekuwaje hunifahamu baada ya mimi kuwa pamoja nanyi muda wote huu? Mtu ye yote ambaye ameniona mimi, amemwona Baba. Sasa inakuwaje unasema, ‘Tuonyeshe Baba’? 10 Je, huamini ya kuwa mimi niko ndani ya Baba yangu, na Baba yangu yuko ndani yangu? Mambo ninayowaambia siyasemi kwa mamlaka yangu mwenyewe, bali yanatoka kwa Baba yangu ambaye anaishi ndani yangu, na ndiye anayetenda haya yote. 11 Niaminini ninapowaambia ya kuwa mimi ni ndani ya Baba yangu na Baba yangu yu ndani yangu. La sivyo, niaminini kwa sababu ya haya mambo ninayotenda. 12 Ninawaambia hakika, mtu ye yote akiniamini ataweza kufanya miujiza kama hii na hata zaidi, kwa kuwa mimi ninakwenda kwa Baba yangu. 13 Kitu cho chote mtakachoomba kwa jina langu, nitawafanyia, ili Baba yangu apate kutukuzwa kwa yale ambayo mimi Mwanae nitawafanyia. 14 Mkiniomba cho chote kwa jina langu nitawafanyia.”

Yesu Anaahidi Roho Mtakatifu

15 “Kama mnanipenda mtatimiza amri zangu. 16 Nami nitam womba Baba, naye atawapeni Msaidizi mwingine akae nanyi siku zote. 17 Huyo ndiye Roho wa Kweli ambaye watu wasioamini hawawezi kumpokea. Watu kama hao hawamwoni wala hawamfahamu. Ninyi mnamfahamu kwa kuwa anakaa ndani yenu na ataendelea kuwa nanyi. 18 Sitawaacha kama yatima. Nitarudi kwenu. 19 Baada ya muda mfupi watu wa ulimwengu hawataniona tena, ila ninyi mta niona; na kwa kuwa mimi ni hai, ninyi pia mtakuwa hai. 20 Wakati huo utakapofika mtajua ya kuwa mimi niko ndani ya Baba yangu na ninyi mko ndani yangu. 21 Mtu anayezishika amri zangu na kuziti miza ndiye anayenipenda. Na mtu anayenipenda, Baba yangu atam penda; nami nitampenda na kujidhihirisha kwake.”

22 Yuda, siyo Iskariote, akamwuliza, “Bwana, itakuwaje ujidhihirishe kwetu tu na si kwa ulimwengu mzima?”

23 Yesu akamjibu, “Mtu akinipenda atashika mafundisho yangu na Baba yangu atampenda, nasi tutafanya makao yetu kwake. 24 Mtu asiyenipenda hayashiki mafundisho yangu na mafundisho niliyowapeni si yangu bali yametoka kwa Baba yangu aliyenituma.

25 “Nimewaambia mambo haya wakati nikiwa bado nipo nanyi. 26 Lakini yule Msaidizi, yaani Roho Mtakatifu, ambaye Baba yangu atamtuma kwenu kwa jina langu, atawafundisha mambo yote, na kuwakumbusha yote niliyowaambia. 27 Ninawaachia amani. Nawapeni amani yangu; amani hii ulimwengu hauwezi kuwapa. Msifadhaike mioyoni mwenu, wala msiogope.

28 Kumbukeni nilivyowaambia, ‘Ninakwenda, na nitarudi.’ Kama kweli mngalinipenda mngefurahi, kwa kuwa nakwenda kwa Baba; na Baba yangu ni mkuu kuliko mimi. 29 Na sasa nimewaambia mambo haya kabla hayajatokea ili yataka potokea mpate kuamini. 30 Sitasema tena mengi nanyi kwa sababu mtawala wa dunia hii anakuja. Yeye hana uwezo juu yangu. 31 Lakini ninatii amri ya Baba ili ulimwengu upate kujua kwamba nampenda Baba.

Simameni tuondoke hapa.’

Mzabibu na Matawi

15 ‘Mimi ni mzabibu wa kweli na Baba yangu ndiye mkulima. Kila tawi ndani yangu lisilozaa matunda, Baba yangu hulikata; na kila tawi lizaalo, yeye hulisafisha ili lipate kuzaa matunda zaidi. Ninyi mmekwisha kuwa safi kwa sababu ya mafundisho nili yowapa. Kaeni ndani yangu nami nikae ndani yenu. Kama vile tawi lisivyoweza kuzaa matunda pasipo kuwa sehemu ya mzabibu, vivyo hivyo, ninyi msipokaa ndani yangu hamwezi kufanya lo lote.

Mimi ni mzabibu; ninyi ni matawi; anayekaa ndani yangu nami ndani yake, huyo huzaa matunda mengi sana; maana pasipo mimi ninyi hamwezi kufanya lo lote. Mtu asipokaa ndani yangu hutupwa nje kama tawi na kunyauka. Matawi hayo hukusanywa na kutupwa motoni, yakateketea. Ninyi mkikaa ndani yangu na maneno yangu yakikaa ndani yenu, ombeni lo lote mtakalo nanyi mtatendewa. Mnapozaa matunda kwa wingi Baba yangu anatukuzwa, na hivyo mnadhihirisha kuwa ninyi ni wanafunzi wangu.

“Kama Baba alivyonipenda mimi, hivyo ndivyo mimi nilivy owapenda ninyi; dumuni katika pendo langu. 10 Mkizishika amri zangu mtakaa ndani ya pendo langu kama mimi nilivyozishika amri za Baba yangu na kukaa katika pendo lake. 11 “Nimewaambia haya kusudi furaha yangu iwe ndani yenu, nanyi mpate kuwa na furaha iliyokamilika. 12 “Amri yangu ni hii: pendaneni kama nilivyowapenda. 13 Hakuna mtu mwenye upendo unaozidi ule wa mtu anayejitoa afe kwa ajili ya rafiki zake. 14 Ninyi ni rafiki zangu ikiwa mtafa nya ninayowaagiza. 15 Siwaiti ninyi watumishi tena kwa sababu mtumishi haelewi shughuli za bwana wake; bali nimewaita rafiki, kwa maana mambo yote niliyoyasikia kutoka kwa Baba yangu nimewa fahamisha. 16 Hamkunichagua, bali mimi nimewachagua ninyi na nimewatuma mwende mkazae matunda, na matunda yenu yapate kudumu, ili lo lote mtakalomwomba Baba katika jina langu, awatimizie. 17 Hii ndio amri yangu: pendaneni.

Ulimwengu Unawachukia Wanafunzi

18 “Kama ulimwengu ukiwachukia, fahamuni kwamba ulinichukia mimi kabla haujawachukia ninyi. 19 Kama mngekuwa watu wa ulim wengu huu, ulimwengu ungeliwapenda. Ulimwengu unawachukia kwa sababu ninyi si wa ulimwengu huu na mimi nimewachagua kutoka katika ulimwengu. 20 “Kumbukeni lile neno nililowaambia, ‘Hakuna mtumishi aliye mkuu kuliko bwana wake.’ Kama wamenitesa mimi na ninyi pia watawatesa; kama wamelishika neno langu na neno lenu watalishika pia. 21 Lakini yote haya watawatendea kwa ajili yangu kwa sababu hawamfahamu Baba yangu ambaye amenituma. 22 Kama sikuja na kusema nao wasingalikuwa na hatia. Lakini sasa hawana udhuru kwa dhambi zao. 23 Mtu ye yote anayenichukia mimi anamchukia na Baba yangu. 24 Kama nilikuwa sikuwafanyia miujiza ambayo haijapata kufanywa na mtu mwingine ye yote, wasingalikuwa na hatia ya dhambi. Lakini wameona miujiza hii na bado wakatuchukia mimi na Baba yangu. 25 “Hali hii imetokea kama ilivyoandikwa katika Sheria kwamba, ‘Walinichukia pasipo sababu.’

Kazi ya Roho Mtakatifu

26 Lakini atakapokuja yule Msaidizi nitakayewapelekea kutoka kwa Baba, yaani yule Roho wa kweli atokaye kwa Baba, yeye atanishuhudia mimi. 27 Na ninyi pia ni mashahidi wangu kwa maana tangu mwanzo mmekuwa pamoja nami.”

16 “Nimewaambia mambo haya yote ili msije mkapoteza imani yenu. Watawatenga na kuwatoa katika ushirika wa masinagogi. Na si hivyo tu, bali utafika wakati ambapo mtu ye yote atakayewaua atadhani kuwa anamtumikia Mungu. Watu watawatendea haya kwa sababu hawamfahamu Baba wala hawanifahamu mimi. Lakini nimew aambia mambo haya kusudi muda huo utakapofika mkumbuke kuwa nili kuwa nimewaambia. Sikuwaambia mambo haya tangu mwanzo kwa sababu nilikuwa pamoja nanyi. “Lakini sasa ninakwenda kwake yeye aliyenituma, wala hakuna mmoja wenu anayeniuliza, ‘Unakwenda wapi?’ Kwa kuwa nimewaambia mambo haya, mioyo yenu imejawa na huzuni. Lakini nawaambia kweli kwamba kuondoka kwangu ni kwa faida yenu kwa maana nisipoondoka, yule Msaidizi hatakuja kwenu. Lakini nikienda nitamtuma aje kwenu. Naye akija atauthibitishia ulim wengu kuhusu dhambi, haki na hukumu. Kuhusu dhambi kwa sababu hawaniamini; 10 kuhusu haki kwa sababu ninakwenda kwa Baba na hamtaniona tena; 11 na kuhusu hukumu kwa sababu mtawala wa ulim wengu huu amekwisha kuhukumiwa.

12 “Nina mambo mengi zaidi ya kuwaambia lakini hamwezi kuy apokea sasa. 13 Akija yule Roho wa kweli atawaongoza muijue kweli yote. Yeye hatanena kwa uwezo wake mwenyewe bali atanena yote atakayosikia. Atawafundisha kuhusu mambo yote yajayo. 14 Atanitukuza mimi, kwa maana atayachukua yaliyo yangu na kuwaambia ninyi. 15 Vyote alivyo navyo Baba ni vyangu, ndio maana nimesema kuwa atachukua yaliyo yangu na kuwaambia ninyi.

Huzuni ya Wanafunzi Itageuka Kuwa Furaha

16 “Baada ya muda mfupi hamtaniona tena; na kisha muda mfupi baadaye mtaniona.” 

17 Baadhi ya wanafunzi wakaulizana, “Ana maana gani asemapo, ‘Baada ya muda mfupi hamtaniona tena na muda mfupi baadaye mtaniona’? Na ana maana gani asemapo, ‘Kwa sababu ninakwenda kwa baba’?” 18 Wakaendelea kuulizana, “Ana maana gani asemapo, ‘muda mfupi?’ Hatuelewi ana maana gani!”

19 Yesu alitambua walilotaka kumwuliza kwa hiyo akawaambia, “Mnaulizana nina maana gani nisemapo, ‘Baada ya muda mfupi ham taniona tena na baada ya muda mfupi mtaniona?’ 20 Ninawaambia yaliyo hakika kwamba mtalia na kuomboleza lakini ulimwengu utafu rahi. Mtahuzunika lakini huzuni yenu itageuka kuwa furaha. 21 Mwanamke akaribiapo kuzaa huwa na huzuni kwa sababu saa yake ya uchungu imefika. Lakini mtoto azaliwapo mama anasahau mateso hayo kwa sababu ya furaha ya kuzaliwa mtoto duniani. 22 Na ninyi sasa mna huzuni lakini nitawaona tena na mtafurahi, wala hakuna atakayewaondolea furaha yenu. 23 Wakati huo hamtaniomba kitu cho chote. Ninawaambia kweli kwamba Baba yangu atawapa lo lote mta kaloomba kwa jina langu. 24 Mpaka sasa hamjaomba lo lote kwa jina langu. Ombeni nanyi mtapewa ili furaha yenu ipate kukamil ika.

25 “Nimewaambia mambo haya kwa mafumbo. Lakini wakati unakuja ambapo sitazungumza nanyi tena kwa mafumbo bali nita waeleza wazi wazi kuhusu Baba yangu. 26 Wakati huo mtaomba kwa jina langu. Wala sisemi kwamba nitamwomba Baba kwa niaba yenu; 27 kwa maana Baba mwenyewe anawapenda kwa sababu mmenipenda mimi na mmeamini kwamba nimetoka kwa Baba. 28 Nilitoka kwa Baba na nimekuja ulimwenguni, tena sasa naondoka ulimwenguni na ninak wenda kwa Baba.”

29 Wanafunzi wake wakasema, “Sasa unazungumza wazi wazi wala si kwa mafumbo. 30 Sasa tumejua kwamba wewe una jua mambo yote wala hakuna haja ya mtu kukuuliza maswali. Kwa hiyo tunaamini kwamba ulitoka kwa Mungu.”

31 Yesu akawajibu, “Sasa mnaamini? 32 Saa inakuja, tena imeshawadia, ambapo mtata wanyika, kila mtu aende nyumbani kwake na kuniacha peke yangu; lakini mimi siko peke yangu kwa sababu Baba yuko pamoja nami.

33 Nimewaambia mambo haya ili mpate kuwa na amani mkiwa ndani yangu. Ulimwenguni mtapata dhiki lakini jipeni moyo, kwa maana mimi nimeushinda ulimwengu.”

Mfano wa Wanawali Kumi

25 Mmoja alimpa talanta tano za fedha, mwingine mbili na mwingine moja; kila mmoja alipewa kwa kadiri ya uwezo wake. Kisha akasa firi. Watano walikuwa wajinga na watano walikuwa na busara. Wale wajinga walichukua taa zao bila akiba ya mafuta; lakini wale wenye busara walichukua taa na mafuta ya akiba. Bwana harusi alipoka wia wale wasichana wote walisinzia, wakalala.

Usiku wa manane zikapigwa kelele: ‘Bwana harusi anakuja! Tokeni nje kumlaki!’

Wasichana wote wakaamka, wakazitengeneza taa zao. Wale wajinga wakawaambia wale wenye busara, ‘Tupatieni mafuta kidogo, taa zetu zinazimika.’

Lakini wenye busara wakajibu, ‘Pengine hayatatutosha sisi na ninyi pia, afadhali nendeni kwa wauza mafuta mkajinunulie wenyewe.’

10 Na walipokuwa wamekwenda kunu nua mafuta, bwana harusi akafika. Wale wasichana waliokuwa tayari wakaingia pamoja naye kwenye karamu ya harusi na mlango uka fungwa.

11 Baadaye wale wasichana wengine pia wakaja, wakaita, ‘Bwana! Bwana! Tufungulie mlango!’ 

12 Bwana harusi akawajibu, ‘Nawaambieni kweli, siwajui.’

13 Kwa hiyo kesheni, kwa sababu hamjui siku wala saa”

Mfano wa Mifuko ya Dhahabu

14 “Pia Ufalme wa mbinguni utafananishwa na mtu aliyekuwa anasafiri, akawaita watumishi wake na kuwakabidhi mali yake. 16 “Yule aliyepewa talanta tano alikwenda mara moja kuzifa nyia biashara akapata talanta tano zaidi. 17 Yule aliyepewa tal anta mbili akafanya hivyo hivyo, akapata mbili zaidi. 18 Lakini yule mtumishi aliyepata talanta moja, alikwenda akachimba shimo akaifukia huko.

19 “Baada ya muda mrefu yule bwana wa hao watumishi alirudi akakagua hesabu za fedha zake alizowaachia. 20 Yule mtumishi aliyepokea talanta tano akaja, akaleta talanta tano zaidi. Akasema, ‘Bwana ulinikabidhi talanta tano, hizi hapa, nimezalisha talanta tano zaidi.’

21 Bwana wake akamwambia, ‘Umefanya vizuri sana, mtumishi mwema na mwaminifu; umekuwa mwaminifu katika machache; nitakupa mamlaka juu ya vitu vingi zaidi. Njoo ufurahi pamoja na bwana wako.’

22 Yule mwenye talanta mbili naye akaja. Akasema, ‘Bwana, ulinikabidhi talanta mbili. Nami nimepata faida, hizi hapa talanta mbili zaidi.’

23 Bwana wake akajibu, ‘Umefanya vizuri sana, mtumishi mwema na mwaminifu; umekuwa mwaminifu katika machache, nami nitakupa mamlaka juu ya vitu vingi zaidi. Njoo ufurahi pamoja na bwana wako.’

24 Kisha yule mtumishi aliyepokea talanta moja akaja, akasema, ‘Bwana, nilijua kwamba wewe ni mtu mgumu, unavuna ambapo hukupanda na kukusanya ambapo hukutawanya mbegu. 25 Kwa hiyo niliogopa, nikaenda nikaificha talanta yako ardhini. Hii hapa mali yako.’

26 Lakini Bwana wake akamjibu, ‘Wewe mtumishi mwovu na mvivu! Ulijua kwamba ninavuna nisipopanda na kukusanya nisipota wanya mbegu? 27 Mbona basi hukuweka fedha zangu benki ili nita kaporudi nizichukue na faida yake? 

28 Mnyang’anyeni hiyo talanta mumpatie yule mwenye talanta kumi.’ 29 Kwa maana kila mtu mwenye kitu ataongezewa, naye atakuwa navyo kwa wingi. Lakini kwa yule asiye na kitu, hata kidogo alicho nacho atanyang’anywa. 30 ‘Mtupeni huyo mtumishi asiyefaa nje kwenye giza, huko kuta kuwa na kilio na kusaga meno.’ ”

Kondoo na Mbuzi

31 “Mwana wa Adamu atakapokuja katika utukufu wake pamoja na malaika wote, ataketi katika kiti chake cha utukufu cha enzi. 32 Watu wa mataifa yote watakusanyika mbele yake, naye atawaten ganisha kama mchungaji anavyotenganisha kondoo na mbuzi. 33 Atawaweka kondoo upande wa kulia na mbuzi upande wa kushoto.

34 Ndipo Mfalme atawaambia wale walioko upande wa kulia, ‘Njooni ninyi mliobarikiwa na Baba yangu, urithini Ufalme mlioandaliwa tangu mwanzo wa dunia. 35 Kwa maana nilikuwa na njaa mkanipa chakula; nilikuwa na kiu mkanipa kitu cha kunywa; nilikuwa mgeni mkanikaribisha; 36 nilikuwa sina nguo, mkanivisha; nilikuwa mgonjwa mkaja kunitazama; na nilikuwa kifungoni mkaja kunitembe lea.’

37 “Kisha wale wenye haki watamjibu, ‘Bwana, ni lini tuli kuona na njaa tukakulisha au ukiwa na kiu tukakupa kitu cha kunywa ? 38 Na ni lini tulikuona ukiwa mgeni tukakukaribisha au ukihitaji nguo tukakuvisha? 39 Na ni lini tulikuona ukiwa mgonjwa au ukiwa kifungoni tukakutembelea?’

40 “Mfalme atajibu, ‘Ninawaambia kweli, kwa jinsi ambavyo mlivyomfanyia mmojawapo wa hawa ndugu zangu walio wadogo, mlini fanyia mimi.’

41 “Kisha atawaambia wale walio kushoto kwake, ‘Ondokeni kwangu ninyi mliolaaniwa, nendeni katika moto wa milele alioan daliwa shetani na malaika zake. 42 Kwa maana nilikuwa na njaa hamkunipa chakula; nilikuwa na kiu na hamkunipa kitu cha kunywa; 43 nilikuwa mgeni wala hamkunikaribisha; nilikuwa uchi hamkuni vika; na nilikuwa mgonjwa na gerezani nanyi hamkuja kunitazama.’

44 “Ndipo wao pia watajibu, ‘Bwana ni lini tulikuona ukiwa na njaa au kiu, au ukiwa mgeni au ukihitaji nguo, au ukiwa mgonjwa na kifungoni na hatukukuhudumia?’

45 “Naye atawajibu, ‘Nawaambieni kweli, kwa jinsi ambavyo hamkumfanyia mmojawapo wa hawa ndugu zangu walio wadogo, hamkuni fanyia mimi.’

46 “Basi hawa wataingia katika adhabu ya milele, lakini wale wenye haki wataingia katika uzima wa milele.”

Mamlaka ya Yesu Yahojiwa

23 Yesu alipoingia tena Hekaluni, makuhani wakuu na wazee walimjia alipokuwa akifundisha, wakamwuliza, “Unafanya mambo haya kwa mamlaka gani na ni nani amekupa mamlaka hayo?”

24 Yesu akawajibu, “Na mimi nitawauliza swali na mkinijibu nami nita waambia ni kwa mamlaka gani ninafanya mambo haya. 25 Ubatizo wa Yohana ulitoka wapi? Mbinguni au kwa watu?”

Wakaanza kubishana kati yao wakisema, “Tukisema ulitoka mbinguni atatuuliza, ‘Mbona basi hamkumwamini?’ 26 Lakini tukisema ulitoka kwa wanadamu, tunaogopa hawa watu, maana wote wanamtambua Yohana kuwa ni nabii.”

27 Kwa hiyo wakamjibu Yesu, “Hatufahamu.”

Naye aka waambia, “Nami sitawaambia ni kwa mamlaka gani ninatenda mambo haya.”

Hadithi ya Wana Wawili

28 ‘Lakini mwaonaje? Mtu mmoja alikuwa na watoto wawili wa kiume. Akamwendea yule wa kwanza akamwambia, ‘Mwanangu, nenda ukafanye kazi kwenye shamba la mizabibu leo.’

29 Yule mwanae akasema, ‘Siendi,’ lakini baadaye akabadili mawazo akaenda. 

30 Kisha yule baba akamwendea yule mwanae mwingine akamwambia vile vile. Yeye akajibu, ‘Nitakwenda baba,’ lakini asiende.

31 Ni yupi kati yao aliyetimiza alivyotaka baba yake?”

 Wakamjibu, “Yule wa kwanza.”

Yesu akawaambia, “Nawaambieni kweli, watoza ushuru na makahaba wanawatangulia kuingia katika Ufalme wa Mungu. 32 Kwa maana Yohana alikuja kwenu kuwaonyesha njia ya haki, lakini hamkumwamini, ila watoza ushuru na makahaba walimwamini. Nanyi hata mlipoona hayo, baadaye hamkutubu na kum wamini.”

Hadithi ya Wapangaji

33 “Sikilizeni mfano mwingine: mtu mmoja mwenye shamba alilima shamba akapanda mizabibu. Akalizungushia ua, na ndani yake akachimba kisima cha kusindikia zabibu; na akajenga mnara. Kisha akalikodisha hilo shamba kwa wakulima fulani, akasafiri kwenda nchi nyingine. 34 “Wakati wa mavuno ulipokaribia aliwatuma watumishi wake kwa hao wakulima kupokea mavuno yake.

35 Wale wakulima wakawaka mata wale watumishi; wakampiga mmoja, wakamwua mwingine na kum piga mawe mwingine. 36 Akatuma watumishi wengine, wengi kuliko wale wa mwanzo. Wale wakulima wakawatendea vile vile. 37 Mwish owe akamtuma mwanae kwao akisema, ‘Bila shaka watamheshimu mwa nangu.’

38 Lakini walipomwona mwanae, waliambiana, ‘Huyu ndiye mrithi. Njooni tumwue tuchukue urithi wake.’ 39 Basi wakamchu kua, wakamtupa nje ya shamba la mizabibu, wakamwua.

40 Sasa, akija yule mwenye shamba, mnadhani atawafanya nini hao waku lima?”

41 Wakamjibu, “Atawaangamiza kabisa hao wadhalimu na kulipangisha shamba lake kwa wakulima wengine ambao watampatia matunda yake wakati wa mavuno.”

42 Yesu akawaambia, “Hamjapata kusoma katika Maandiko kwamba: 

‘Lile jiwe walilokataa wajenzi limekuwa jiwe kuu la pembeni; Bwana ndiye amefanya jambo hili nalo ni zuri ajabu machoni petu’? (Zaburi 118:22,23)

43 Kwa hiyo ninawaambia, Ufalme wa Mungu utaondolewa kwenu na watapewa watu wawezao kutoa matunda yake.” [ 44 “Na ambaye ataanguka kwenye jiwe hili atavunjika vipande vipande, lakini yule litakayemwangukia atasagika sagika.”]

45 Makuhani wakuu na Mafarisayo waliposikia mifano yake, walitambua kuwa alikuwa akiwasema wao. 46 Wakatafuta njia ya kumkamata lakini waliogopa ule umati wa watu kwa kuwa wao walim tambua Yesu kuwa nabii.

Hadithi ya Chakula cha jioni cha Harusi

22 Yesu akazungumza nao tena kwa kutumia mifano, akasema, “Ufalme wa mbinguni unaweza kufananishwa na mfalme mmoja ali yemwandalia mwanae karamu ya harusi. Akawatuma watumishi wake wakawaite wageni walioalikwa lakini wakakataa kuja.

Akawatuma watumishi wengine akisema, ‘Waambieni waalikwa kwamba karamu iko tayari, nimekwisha chinja fahali wangu na ng’ombe wanono kwa ajili yenu, karibuni karamuni.’

Lakini waalikwa wakadharau, mmoja akaenda shambani kwake, mwingine akaenda kwenye miradi yake, na wengine wakawakamata wale watumishi wakawatendea mambo ya aibu na kuwaua. “Yule mfalme akakasirika, akapeleka jeshi lake likawaanga miza wale wauaji na kuteketeza mji wao.

Kisha akawaambia watum ishi wake, ‘Karamu ya harusi ni tayari, lakini wale niliowaalika hawakustahili kuja karamuni. Kwa hiyo nendeni katika njia panda mkawaalike harusini wote mtakaowakuta.’ 10 Wale watumishi wakaenda mabarabarani wakawakusanya wote waliowakuta, wema na wabaya. Ukumbi wa sherehe ya harusi ukajaa wageni.

11 “Lakini mfalme alipoingia kutazama wageni, alimwona mle ndani mtu mmoja ambaye hakuwa amevaa vazi la harusi. 12 Mfalme akamwuliza, ‘Rafiki, umeingiaje humu bila vazi la harusi?’ Yule mtu hakuwa na la kusema.

13 Basi mfalme akawaambia watumishi wake, ‘Mfungeni mikono na miguu mkamtupe nje kwenye giza. Huko kutakuwa na kilio na kusaga meno.’

14 Kwa maana walioitwa ni wengi lakini walioteuliwa ni wachache.”

Je, Ni Sawa Kumlipa Kaisari Ushuru wa Kifalme?

15 Mafarisayo walifanya mbinu za kumtega Yesu katika mafundi sho yake. 16 Wakatuma wanafunzi wao pamoja na Maherode wakam wambie, “Mwalimu, tunajua kwamba wewe ni mtu wa haki na unafundisha njia za Mungu kwa uaminifu bila kumjali mtu, kwa maana cheo si kitu kwako. 17 Basi tuambie, wewe unaonaje? Ni halali, au si halali kulipa kodi kwa Kaisari?”

18 Yesu alifahamu hila yao kwa hiyo akawaambia, “Ninyi wanafiki, kwa nini mnajaribu kunitega? 19 Nionyesheni sarafu mnayolipia kodi.” Wakamletea sarafu. 20 Yesu akawauliza, “Picha hii na sahihi hii ni za nani?”

21 Wakamjibu, “Ni za Kaisari.”

Basi Yesu akawaambia, “Mpeni Kaisari yaliyo ya Kais ari; na ya Mungu mpeni Mungu.”

22 Waliposikia haya wakashangaa; wakamwacha, wakaondoka.

Ndoa Wafu Watakapofufuka

23 Siku hiyo hiyo Masadukayo, wale wanaoamini kwamba wafu hawafufuki, walikuja kwa Yesu wakamwuliza, 24 “Mwalimu, Musa alitufundisha kwamba mtu akifariki pasipo kupata watoto, ndugu yake amwoe huyo mjane ili ampatie kaka yake watoto. 25 Hapa kwetu walikuwapo ndugu saba. Wa kwanza alioa mke, kisha akafariki na kwa kuwa hakuwa na watoto, yule mjane alichukuliwa na ndugu yake. 26 Ikatokea hivyo hivyo kwa yule ndugu wa pili hadi wote saba wakamwoa huyo mjane bila kupata watoto. 27 Baadaye, yule mjane naye akafariki. 28 Sasa tuambie, siku ile ya ufufuo, ata hesabiwa kuwa ni mke wa nani? Maana aliolewa na wote saba!”

29 Yesu akawajibu, “Mnakosea kwa sababu hamjui Maandiko wala uwezo wa Mungu. 30 Wakati wa ufufuo, watu hawataoa wala kuolewa; kwa maana watakuwa kama malaika wa mbinguni. 31 Na kuhusu ufufuo wa wafu, hamjasoma Mungu alivyowaambia kwamba, 32 ‘Mimi ni Mungu wa Ibrahimu, Mungu wa Isaka na Mungu wa Yakobo’? Yeye si Mungu wa wafu bali ni Mungu wa walio hai.”

33 Ule umati wa watu waliposikia hayo, walishangazwa sana na mafund isho yake.

Amri Muhimu Sana

34 Mafarisayo waliposikia kwamba Yesu alikuwa amewanyamazi sha Masadukayo, walikutana wakamjia pamoja. 35 Mmoja wao, mtaalamu wa sheria akajaribu kumtega kwa kumwuliza, 36 “Mwali mu, ni amri ipi iliyo kuu kuliko zote?”

37 Yesu akamjibu, “Mpende Bwana Mungu wako kwa moyo wako wote, na kwa roho yako yote na kwa akili zako zote.’ 38 Hii ndio amri kuu, tena ni ya kwanza. 39 Na ya pili inafanana nayo, nayo ni hii: ‘Mpende jirani yako kama nafsi yako.’ 40 Amri hizi mbili ndio msingi wa sheria zote na Maandiko ya manabii.”

Masihi Ni Mwana wa Nani?

41 Mafarisayo walipokuwa pamoja Yesu aliwauliza, 42 “Mnaonaje kuhusu Kristo? Yeye ni mwana wa nani?”

Wakamjibu, “Yeye ni mwana wa Daudi.”

43 Akawaambia, “Inakuwaje basi kwamba Daudi anapozungumza kwa Roho anamwita Kristo ‘Bwana,’ kwa kusema,

44 ‘Bwana alimwam bia Bwana wangu: keti upande wangu wa kulia mpaka nitakapowaweka adui zako chini ya miguu yako.’

45 Kama Daudi anamwita ‘Bwana 46 Hakuna aliyeweza kumjibu Yesu hata neno moja. Na tangu siku hiyo hakuna aliyethubutu tena kum wuliza maswali.

Onyo Dhidi ya Kufanya Mambo kwa Sababu Zisizofaa

23 Kisha Yesu akawaambia ule umati wa watu pamoja na wana funzi wake: “Walimu wa sheria na Mafarisayo wamechukua nafasi ya Musa, kwa hiyo watiini na kufanya yote wanayowaambia mfa nye. Lakini msifuate matendo yao; kwa sababu hawatendi yale wanayohubiri. Wao hufunga mizigo mikubwa na kuwabebesha watu, lakini wao wenyewe hawajaribu hata kunyoosha kidole kuisogeza!

“Wao hufanya mambo yao yote ili waonekane na watu. Wanavaa vipande vipana vya ngozi vilivyoandikwa sheria na kurefusha zaidi pindo za mavazi yao ya sala. Wanapenda kukaa viti vya wageni wa heshima karamuni na viti vya mbele katika masinagogi. Hupenda kuamkiwa masokoni na kuitwa ‘Rabi.’

“Lakini ninyi msipende kuitwa ‘Rabi’ kwa sababu mnaye rabi mmoja, na ninyi nyote ni ndugu. Na msimwite mtu ye yote hapa duniani ‘baba’ kwa maana mnaye Baba mmoja, naye yuko mbinguni. 10 Hali kadhalika msipende kuitwa ‘mabwana’ kwa maana mnaye Bwana mmoja tu, yaani Kristo. 11 Aliye mkuu kuliko ninyi nyote atakuwa mtumishi wenu. 12 Ye yote anayejikuza atashushwa; na ye yote anayejinyenyekeza atainuliwa.

Ole gani kwa Walimu wa Sheria na Mafarisayo

13 “Lakini ole wenu walimu wa sheria na Mafarisayo, ninyi wanafiki! Kwa maana mnafungia watu milango ya Ufalme wa mbinguni. Ninyi wenyewe hamuingii humo, wala hamruhusu wale ambao wange penda kuingia waingie. [14 “Ole wenu walimu wa sheria na Mafarisayo, ninyi wana fiki! Mnadhulumu nyumba za wajane, na kwa kujionyesha kuwa wema, mnasali sala ndefu. Kwa hiyo adhabu yenu itakuwa kubwa zaidi.”]

15 “Ole wenu walimu wa sheria na Mafarisayo, ninyi wana fiki! Mnasafiri baharini na nchi kavu ili kumfanya mtu mmoja awe mfuasi wa dini yenu, lakini baada ya kumpata, mnamfanya astahili kwenda Jehena mara mbili zaidi yenu!

16 “Ole wenu viongozi vipofu! Ninyi mnasema, ‘Mtu akiapa kwa Hekalu, kiapo hicho si kitu; lakini mtu akiapa kwa dhahabu iliyoko Hekaluni, itambidi atimize kiapo hicho.’ 17 Ninyi vipofu wajinga! Ni kipi kilicho bora zaidi, ni ile dhahabu au ni Hekalu ambalo ndilo linafanya dhahabu hiyo kuwa takatifu? 18 Pia mnasema, ‘Mtu akiapa kwa madhabahu, si kitu, lakini mtu akiapa kwa sadaka iliyoko madhabahuni itambidi atimize kiapo hicho.’ 19 Ninyi vipofu! Ni kipi bora zaidi, sadaka, au madhabahu ambayo ndio inafanya sadaka hiyo kuwa takatifu? 20 Kwa hiyo mtu anayeapa kwa madhabahu, anaapa kwa hiyo madhabahu na vitu vyote vilivyoko juu yake. 21 Na mtu anapoapa kwa Hekalu, anaapa kwa hilo Hekalu na huyo aishie ndani yake. 22 Naye anayeapa kwa mbingu anaapa kwa kiti cha enzi cha Mungu na kwa yeye aketiye juu ya kiti hicho.

23 “Ole wenu walimu wa sheria na Mafarisayo, ninyi wana fiki! Kwa maana mnatoa fungu la kumi la mnanaa, na bizari na jira; lakini mmepuuza mambo makuu zaidi ya sheria: haki, huruma na imani. Haya mlipaswa kuyafanya bila kusahau yale mengine. 24 Ninyi viongozi vipofu, mnachuja nzi lakini mnameza ngamia!

25 “Ole wenu walimu wa sheria na Mafarisayo, ninyi wana fiki! Kwa maana mnasafisha kikombe na sahani kwa nje lakini ndani mmejaa ulafi na unyang’anyi. 26 Ninyi Mafarisayo vipofu! Kwanza safisheni kikombe na sahani kwa ndani, ndipo nje patakuwa safi.

27 “Ole wenu, walimu wa sheria na Mafarisayo, ninyi wana fiki! Mnafanana na makaburi yaliyopakwa chokaa ambayo kwa juu yanaonekana maridadi lakini ndani yamejaa mifupa ya wafu na kila aina ya uchafu. 28 Hali kadhalika, nje ninyi mnaonekana kwa watu kuwa wenye haki, lakini kwa ndani mmejaa unafiki na uovu.

29 “Ole wenu, walimu wa sheria na Mafarisayo, ninyi wana fiki! Mnajenga makaburi ya manabii na kupamba makaburi ya wenye haki 30 mkisema, ‘Kama tungaliishi wakati wa baba zetu tusingel ishiriki katika kuwaua manabii !’ 31 Kwa kusema hivyo mnakiri kwamba ninyi ni wana wa wale waliowaua manabii. 32 Haya basi, kamilisheni hiyo kazi waliyoianza baba zenu!

33 Ninyi nyoka, ninyi kundi la nyoka! Mtaepukaje hukumu ya Jehena? 34 Kwa sababu hiyo nawapelekea manabii na wenye hekima na walimu. Baadhi yao mtawaua na kuwatundika msalabani, wengine mtawapiga mijeledi katika masinagogi yenu na wengine mtawatesa toka mji mmoja hadi mji mwingine. 35 Na kwa hiyo damu ya wote wenye haki ambayo imemwagwa hapa duniani, tangu damu ya Abeli, ambaye alikuwa hana hatia, hadi damu ya Zakaria mwana wa Barakia ambaye mlimwua kati kati ya Patakatifu na madhabahu, itakuwa juu yenu. 36 Nawaambia kweli haya yote yatatokea wakati wa kizazi hiki.”

37 “Ninyi watu wa Yerusalemu; mnawaua manabii na kuwapiga mawe wale waliotumwa kwenu! Nilitamani sana kuwakusanya wana wenu kama vile kuku akusanyavyo vifaranga vyake chini ya mbawa zake, lakini hamkutaka! 38 Tazama nyumba yenu imeachwa tupu na ukiwa. 39 Kwa maana nawahakikishia kuwa, hamtaniona tena mpaka siku ile mtakaposema: ‘Amebarikiwa yeye anayekuja kwa jina la Bwana. (Zaburi 118:26)

Mzabibu umesinyaa, mtini nao umevia;
    Nao mkomamanga na mtende na mtofaa;
Naam, miti yote ya mashamba imekauka;
    Maana furaha imekauka katika wanadamu.

Yoeli 1:12

 “Nami nimewapiga kwa ukavu na koga; 
    wingi wa bustani zenu na mashamba yenu ya mizabibu,
na mitini yenu na mizeituni yenu imeliwa na tunutu;
    Lakini hamkunirudia mimi,”
    asema Bwana.

Amosi 4:9

Je! Mbegu ingali ghalani? Naam, huo mzabibu, wala mtini, wala mkomamanga, wala mzeituni, haikuzaa kitu; tangu siku hii ya leo nitawabariki.

Hagai 2:19

Na jeshi lote la mbinguni litafumuliwa, na mbingu zitakunjwa kama karatasi, na jeshi lao lote litanyauka kama vile jani la mzabibu linyaukavyo na kupukutika, na kama jani la mtini linyaukavyo na kupukutika.

Isaya 34:4

 Nitawaangamiza kabisa, asema Bwana; hapana zabibu katika mizabibu, wala tini katika mitini, hata jani lake litanyauka; na vitu vile nilivyowapa vitawapotea.

Yeremia 8:13

41 Esau akamchukia Yakobo kwa ajili ya ule mbaraka babaye aliombarikia. Esau akasema moyoni mwake, Siku za kumlilia baba yangu zinakaribia, ndipo nitakapomwua ndugu yangu Yakobo.

42 Rebeka akaarifiwa maneno ya Esau, mwanawe mkubwa. Akapeleka mtu kumwita Yakobo, mwanawe mdogo, akamwambia, Tazama, katika habari zako Esau, ndugu yako, anajifariji moyo wake, maana anakusudia kukuua. 43 Na sasa, mwanangu, sikia sauti yangu, uondoke, ukimbilie kwa Labani, ndugu yangu huko Harani; 44 ukae kwake siku chache, hata ghadhabu ya ndugu yako igeuke; 45 hata ikuondokee ghadhabu ya ndugu yako, akasahau uliyomtenda. Ndipo nitakapopeleka watu kukuchukua kutoka huko. Kwa nini nifiwe nanyi nyote wawili siku moja?

46 Rebeka akamwambia Isaka, Rohoni mwangu sina raha kwa sababu ya hao binti za Hethi. Kama Yakobo akitwaa mke katika binti za Hethi, kama hawa binti za nchi, maisha yangu yatanifaidia nini?

28 Basi Isaka akamwita Yakobo, akambariki, akamwagiza akamwambia, Usitwae mke wa binti za Kanaani. Ondoka, uende Padan-aramu, mpaka nyumba ya Bethueli baba ya mama yako, ukajitwalie huko mke katika binti za Labani, ndugu wa mama yako. Na Mungu Mwenyezi, akubariki, akuzidishe, na kukuongeza, ili uwe mkutano wa makabila. Akupe mbaraka wa Ibrahimu, wewe na uzao wako pamoja nawe, upate kuirithi nchi ya kusafiri kwako, Mungu aliyompa Ibrahimu. Basi Isaka akampeleka Yakobo, naye akaenda Padan-aramu, kwa Labani, mwana wa Bethueli, Mshami, ndugu wa Rebeka, mama yao Yakobo na Esau.

Utangulizi wa Mahubiri ya Mlimani

5 Yesu alipoona umati wa watu, alipanda mlimani akaketi chini. Wanafunzi wake wakamjia, naye akaanza kuwafundisha,

Vipimo

akisema:

“Wamebarikiwa walio maskini wa roho; maana Ufalme wa mbin guni ni wao. 

Wamebarikiwa wanaoomboleza; maana watafarijiwa. 

Wamebarikiwa walio wapole; maana watairithi nchi. 

Wamebari kiwa wenye hamu ya kutenda haki; maana wataridhishwa. 

Wamebari kiwa walio na huruma; maana nao watahurumiwa. 

Wamebarikiwa walio na moyo safi; maana watamwona Mungu. 

Wamebarikiwa walio wapatanishi; maana wataitwa wana wa Mungu. 

10 Wamebarikiwa wanaoteswa kwa kutenda haki; maana Ufalme wa mbinguni ni wao.

11 Mmebarikiwa ninyi wakati watu watakapowatukana na kuwatesa na kuwasingizia maovu kwa ajili yangu. 12 Shangilieni na kufurahi, kwa maana zawadi yenu huko mbinguni ni kubwa; kwa kuwa ndivyo walivyowatesa manabii waliowatangulia ninyi.

Chumvi na Mwanga

13 “Ninyi ni chumvi ya ulimwengu. Lakini chumvi ikipoteza ladha yake, haiwezekani kuwa chumvi tena. Haifai kwa kitu cho chote, ila kutupwa nje ikanyagwe na watu.

14 “Ninyi ni nuru ya ulimwengu. Mji uliojengwa kwenye mlima haufichiki. 15 Wala hakuna mtu anayewasha taa kisha akaifunika. Badala yake, huiweka mahali pa juu ili itoe mwanga kwa kila mtu aliyemo ndani ya nyumba. 16 Hali kadhalika, nuru yenu iwaangazie watu ili waone matendo yenu mema wamtukuze Baba yenu aliye mbin guni.’

Utimilifu wa Sheria

17 “Msidhani kwamba nimekuja kufuta sheria ya Musa na mafundisho ya manabii. kwamba mpaka mbingu na dunia zitaka potoweka, hakuna hata herufi moja ya sheria itakayopotea mpaka shabaha yake ikamilike. 19 Kwa hiyo ye yote atakayelegeza hata mojawapo ya amri ndogo kuliko amri zote na akawafundisha wengine kufanya hivyo, ataitwa mdogo kabisa katika Ufalme wa mbinguni. Sikuja kuzifuta bali kuzitimiza. 18 Kwa maana ninawaambia hakika Lakini atakayetii amri hizi na kuwafundisha wengine kuzitii a taitwa mkuu katika Ufalme wa mbinguni. 20 Kwa maana nawaambieni, ikiwa haki yenu haitazidi haki ya waandishi wa sheria na Mafari sayo, hamtaingia katika Ufalme wa mbinguni kamwe.”

Mauaji

21 “Mmesikia walivyowafundisha watu wa zamani kwamba, ‘Usiue; na ye yote atakayeua atastahili hukumu.’ 22 Lakini mimi nawaambia kwamba, ye yote atakayemkasirikia ndugu yake atasta hili hukumu; na ye yote atakayemtukana ndugu yake, atashtakiwa katika baraza; na ye yote atakayemwambia ndugu yake, ‘Wewe mjinga,’ atastahili hukumu ya moto wa Jehena.

23 “Basi, kama ulikuwa tayari kutoa sadaka yako madhaba huni, ukakumbuka kuwa ndugu yako amekukasirikia, 24 acha sadaka yako hapo hapo, uende kwanza ukapatane naye, kisha urudi kumtolea Mungu sadaka yako.

25 “Mtu akikushtaki, patana naye kabla hamjafika mahaka mani; ili mshtaki wako asije akakukabidhi kwa hakimu, na hakimu akamwamuru askari akufunge gerezani; 26 nami nawaambia hakika, hutatoka huko mpaka deni lako lote litakapolipwa.”

Uzinzi

27 “Mmesikia walivyowafundisha watu wa zamani kwamba, ‘Usi zini’. 28 Lakini mimi nawaambia: ye yote atakayemwangalia mwa namke kwa kumtamani, amekwisha kuzini naye moyoni mwake. 29 Jicho lako la kulia likikufanya utende dhambi, ling’oe ulitu pilie mbali. Ni afadhali upoteze sehemu ya mwili wako kuliko mwili mzima utupwe Jehena. 30 Na kama mkono wako wa kuume ukiku fanya utende dhambi, ukate uutupilie mbali. Ni afadhali upoteze sehemu ya mwili wako kuliko mwili mzima utupwe Jehena.

Talaka

31 “Pia mliambiwa kwamba, ‘Mtu ye yote anayemwacha mkewe ampe talaka.’ 32 Lakini mimi nawaambia, ye yote atakayempa mkewe talaka isipokuwa kwa kosa la uasherati, anamfanya mkewe mzinzi. Na ye yote atakayemwoa mwanamke aliyepewa talaka anazini.”

Viapo

33 “Tena mmesikia watu wa kale waliambiwa kwamba, ‘Usi vunje kiapo chako bali umtimizie Mungu kama ulivyoapa kutenda.’ 34 Lakini mimi nawaambia, msiape kabisa, ama kwa mbingu, kwa sababu ni kiti cha enzi cha Mungu, 35 au kwa ardhi, kwa sababu ndipo mahali pake pa kuwekea miguu, au kwa Yerusalemu kwa sababu ndio mji wa Mfalme mkuu. 36 Na msiape kwa vichwa vyenu kwa sababu hamwezi kugeuza hata unywele mmoja kuwa mweupe au mweusi. 37 Ukisema ‘Ndio’ basi iwe ‘Ndio’; na ukisema ‘Hapana’ basi iwe ‘ Hapana.’ Lo lote zaidi ya haya hutoka kwa yule mwovu.”

Jicho kwa Jicho

38 “Mmesikia kuwa watu zamani walikuwa wakisema, ‘Jicho kwa jicho na jino kwa jino.’ 39 Lakini mimi nawaambia, msishindane na mtu mwovu. Lakini mtu akikupiga kwenye shavu la kulia, mgeuzie na shavu la kushoto pia; 40 na kama mtu akitaka kukushtaki achukue shati lako, mwachie achukue na koti pia. 41 Na kama mtu akikulazimisha uende kilometa moja naye, fanya zaidi, nenda naye kilometa mbili. 42 Mtu akikuomba kitu mpe, na usikatae kumsaidia mtu anayetaka kukukopa.”

Upendo kwa Maadui

43 “Mmesikia kuwa watu zamani walikuwa wakisema, ‘Umpende jirani yako na umchukie adui yako.’ 44 Lakini mimi ninawaambia, wapendeni maadui zenu na waombeeni wanaowatesa, 45 ili mpate kuwa watoto wa Baba yenu aliye mbinguni. Kwa maana yeye huwaanga zia jua lake watu waovu na watu wema; na pia huleta mvua kwa wenye haki na wasio haki. 46 Kama mkiwapenda wanaowapenda tu, mtapata thawabu gani? Hata wenye dhambi hufanyiana hivyo. 47 Na kama mkiwasalimu ndugu zenu tu, mnafanya nini zaidi ya wengine? Hata watu wa mataifa wasiomjua Mungu, hufanya hivyo. 48 Kwa hiyo inawapasa ninyi muwe wakamilifu kama Baba yenu wa mbinguni alivyo mkamilifu.”

Kutoa kwa Wahitaji

6 “Angalieni msitende mema mbele ya watu ili muonekane na watu. Kwa maana mkifanya hivyo hamtapata thawabu itokayo kwa Baba yenu aliye mbinguni.

“Kwa hiyo mnapowasaidia maskini msitangaze kwa tarumbeta kama wafanyavyo wanafiki katika masinagogi na mitaani ili wasi fiwe na watu. Nawaambia wazi, wao wamekwisha pata tuzo yao. Lakini ninyi mnapotoa sadaka, fanyeni kwa siri, hata mkono wako wa kushoto usijue mkono wako wa kulia unafanya nini; ili sadaka yako iwe ni siri. Naye Baba yako wa mbinguni anayeona sirini ata kupa thawabu.”

Maombi

“Na mnaposali, msiwe kama wanafiki; maana wao wanapenda kusimama na kusali katika masinagogi na kando ya barabara ili waonekane na watu. Nawaambieni kweli, wao wamekwisha kupata tuzo yao. Unaposali, nenda chumbani kwako ufunge mlango na umwombe Baba yako aliye sirini. Na Baba yako aonaye sirini atakupa tha wabu. “Mnaposali msirudie maneno yale yale kama wafanyavyo watu wa mataifa wasiomjua Mungu. Kwa maana wao hudhani kwamba watasi kilizwa kwa sababu ya wingi wa maneno yao. Msiwe kama wao, kwa sababu Baba yenu anajua mahitaji yenu hata kabla hamjaomba.”

Basi msalipo ombeni hivi:

‘Baba yetu uliye mbinguni
jina lako litukuzwe.
10 Ufalme wako uje,
mapenzi yako yafanyike
hapa duniani kama huko mbinguni.
11 Utupatie leo riziki yetu ya kila siku.
12 Na utusamehe makosa yetu
     kama sisi tulivyokwisha kuwa samehe waliotukosea.
13 Na usitutie majaribuni,
     bali utuokoe kutokana na yule mwovu.

14 Kama mkiwasamehe watu makosa yao, Baba yenu wa mbinguni atawasamehe na ninyi; 15 lakini msipowasamehe watu makosa yao, Baba yenu hatawasamehe makosa yenu.

Kufunga

16 “Mnapofunga, msionyeshe huzuni kama wafanyavyo wanafiki. Maana wao hukunja nyuso zao ili kujionyesha. Nawaambieni kweli kwamba wao wamekwisha kupata tuzo yao. 17 Lakini mnapofunga, jipakeni mafuta kichwani na kuosha nyuso zenu 18 ili kufunga kwenu kusijulikane kwa mtu ila Baba yenu aliye sirini; na Baba yenu aonaye katika siri atawapa thawabu.” Akiba Ya Mbinguni.

Hazina Mbinguni

19 “Msijiwekee mali nyingi duniani ambapo wadudu na kutu huharibu na wezi huvunja na kuiba. 20 Lakini jiwekeeni mali mbinguni ambapo wadudu na kutu hawaharibu na wezi hawavunji na kuiba. 21 Kwa sababu pale akiba yako ilipo ndipo moyo wako uta kapokuwa.”

22 “Jicho ni taa ya mwili. Kama jicho lako ni zuri, mwili wako wote utakuwa na nuru. 23 Lakini kama jicho lako ni bovu, mwili wako wote utakuwa na giza. Kwa hiyo kama nuru iliyomo ndani yako ni giza, hakika utakuwa na giza la kutisha.”

24 “Hakuna mtu anayeweza kuwatumikia mabwana wawili, kwa sababu, ama atamchukia mmoja na kumpenda mwingine, au atamthami ni mmoja na kumdharau mwingine. Huwezi kumtumikia Mungu na mali.”

Usijali

25 “Kwa hiyo nawaambia, msiwe na wasiwasi kuhusu maisha yenu: mtakula nini au mtakunywa nini; au kuhusu miili yenu: mvae nini. Kwani maisha si zaidi ya chakula? Na mwili zaidi ya mavazi? 26 Waangalieni ndege wa angani: wao hawapandi wala kuvuna wala kuweka cho chote ghalani. Lakini Baba yenu wa mbinguni anawali sha. Je ninyi, si wa thamani zaidi kuliko ndege? 27 Ni nani kati yenu ambaye kwa kujihangaisha kwake anaweza kujiongezea hata saa moja zaidi kwenye maisha yake?

28 “Na kwa nini mnahangaikia mavazi? Angalieni maua ya mwi tuni yanavyostawi. Hayafanyi kazi wala hayashoni nguo. 29 Lakini nawaambia, hata mfalme Sulemani katika ufahari wake wote hakuwahi kuvikwa kama mojawapo la maua hayo. 30 Lakini ikiwa Mungu anay avisha hivi maua ambayo leo yapo na kesho yanatupwa motoni, je, hatawavisha ninyi vizuri zaidi, enyi watu wenye imani haba? 31 Kwa hiyo msiwe na wasiwasi mkisema, ‘Tutakula nini?’ au ‘Tutakunywa nini?’ au ‘Tutavaa nini?’ 32 Mambo haya ndio yanay owahangaisha watu wa mataifa wasiomjua Mungu; na Baba yenu wa mbinguni anafahamu kwamba mnahitaji yote hayo. 33 Lakini uta futeni kwanza Ufalme wa mbinguni na haki yake, na haya yote mtaongezewa. 34 Kwa hiyo msihangaike kuhusu kesho, kwa sababu kesho itajihangaikia yenyewe. Kila siku ina shida zake za kutosha.”

Kuwahukumu Wengine

7 Usihukumu ili na wewe usihukumiwe. Kwa maana hukumu uta kayotamka juu ya wenzako ndio itakayotumiwa kukuhukumu, na kipimo utakachotoa ndicho utakachopokea.

Kwa nini unaangalia kijiti kidogo kilichomo katika jicho la ndugu yako na wala huoni pande la mti lililoko jichoni mwako? Au unawezaje kumwambia ndugu yako, ‘Hebu nikutoe uchafu jichoni mwako,’ wakati jichoni mwako mna pande kubwa? Mnafiki wewe! Toa kwanza pande lililoko jichoni mwako, ndipo utaweza kuona vema, upate kukitoa kipande kilichoko ndani ya jicho la ndugu yako.

“Msiwape mbwa vitu vitakatifu; na msitupe lulu zenu mbele ya nguruwe wasije wakazikanyaga kanyaga na halafu wawageukie na kuwashambulia.”

Uliza, Tafuta, Gonga

“Ombeni nanyi mtapewa. Tafuteni nanyi mtapata; bisheni hodi nanyi mtafunguliwa mlango. Kwa sababu kila aombaye hupewa; naye atafutaye hupata; na abishaye hodi atafunguliwa mlango.

“Au ni nani kati yenu ambaye kama mwanae akimwomba mkate atampa jiwe? 10 Au akimwomba samaki atampa nyoka? 11 Ikiwa ninyi mlio waovu mnafahamu jinsi ya kuwapa watoto wenu zawadi nzuri, ni mara ngapi zaidi Baba yenu wa mbinguni atawapa vitu vizuri wale wamwombao? 12 Kwa hiyo cho chote ambacho ungependa watu wakutendee, na wewe watendee vivyo hivyo. Hii ndio maana ya sheria ya Musa na Maandiko ya manabii.”

Milango Nyembamba na Mipana

13 “Ingieni kwa kupitia mlango mwembamba; kwa maana mlango mpana na njia rahisi huelekea kwenye maangamizo, na watu wanaopitia huko ni wengi. 14 Lakini mlango mwembamba na njia ngumu huelekea kwenye uzima, na ni wachache tu wanaoiona.”

Manabii wa Kweli na wa Uongo

15 “Jihadharini na manabii wa uongo wanaowajia wakiwa wamevaa ngozi ya kondoo, kumbe ndani ni mbwa mwitu wakali. 16 Mtawatambua kwa matunda yao. Je, unaweza kuchuma zabibu kwenye miiba au tini kwenye michongoma? 17 Vivyo hivyo mti mzuri huzaa matunda mazuri na mti mbaya huzaa matunda mabaya. 18 Mti mzuri hauwezi kuzaa matunda mabaya na mti mbaya hauwezi kuzaa matunda mazuri. 19 Kila mti usiozaa matunda mazuri hukatwa katwa na kutupwa motoni. 20 Hivyo, mtawatambua kwa matunda yao.”

Wanafunzi wa Kweli na wa Uongo

21 “Si kila mtu anayesema, ‘Bwana, Bwana,’ ambaye ataingia katika Ufalme wa mbinguni ila ni wale wanaofanya mapenzi ya Baba yangu aliye mbinguni. 22 Siku ile itakapofika wengi wata niambia, ‘Bwana, Bwana, hatukutoa unabii na kufukuza pepo kwa jina lako; na kufanya miujiza mingi ya ajabu kwa jina lako?’ 23 Ndipo nitawaambia wazi, ‘Sikuwafahamu kamwe. Ondokeni kwangu ninyi watenda maovu!’

Wajenzi Wenye Busara na Wapumbavu

24 “Basi, kila anayesikiliza haya maneno yangu na kuyate keleza, atafanana na mtu mwenye busara aliyejenga nyumba yake kwenye mwamba. 25 Mvua ikanyesha, mafuriko yakaja na upepo uka vuma ukaipiga nyumba hiyo, lakini haikuanguka kwa sababu ili jengwa kwenye msingi imara juu ya mwamba. 26 Na kila anayesikia haya maneno yangu asiyafuate, atafanana na mtu mjinga aliyejenga nyumba yake kwenye mchanga. 27 Mvua ikanyesha, yakatokea mafu riko, na upepo ukavuma ukaipiga hiyo nyumba, nayo ikaanguka kwa kishindo kikubwa.”

28 Na Yesu alipomaliza kusema maneno haya, umati wa watu waliomsikiliza walishangaa sana, 29 kwa sababu alifundisha kama mtu mwenye mamlaka, na si kama walimu wao wa sheria.